50 CENT AMDISS P.DIDY

Rapa 50 cent amekuwa akisifika kwa kupenda ma-bifu na wasanii wenzake ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakipelekea uhasama baina yao. Safari hii hitmaker huyo wa In Da Club, amemdiss mmilikiwa studio za bad Boys, Sean Combs A.K.A P.Diddy kwa kumwambia kuwa hana sifa za kuitwa msanii. Akichezesha taya kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Dj Enuff, 50 Cent…

PICHA : BIRTHDAY YA MIAKA 2 YA EFM 93.7 NDANI YA MAISHA BASEMENT

  Kituo maarufu mjini cha utangazaji, Efm, kinachopatikana kwenye masafa ya 93.7 jijini Dar es salaam, mwanzoni mwa juma hili(Jumatatu) waliangusha bonge la birthday katika kusherekea kutimiza miaka 2 tangu kuzaliwa kwake ndani ya ukumbi wa burudani wa maisha Basement. Wahenga wanakwambia mwenye macho haambiwi tazama, nisikuchoshe sana fanya kutazama hapo chini ujionee mambo yalivyokuwa.…

TAZAMA MUONEKANO MPYA WA JUSTIN BIEBER

Supastaa daraja la kwanza asiyehishiwa vituko kila kukicha, Justin Bieber, amewa-suprise mashabiki wake kwa kutokelezea na mtindo mpya wa nywele. Muimbaji huyo Raia wa Canada aliwashangaza mashabiki wake wakati alipokuwa aki-perform kwenye sherehe za utoaji Tuzo za iHeartRadio akiwa amesokota nywele zake(Dreadrocks) na kumfanya kuwa kivutio kikubwa jukwaani. katika Tuzo hizo, Bieber alifanikiwa kunyakuwa Tuzo…

BASATA WAFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO ‘SHIKA ADABU YAKO’

Baraza la Sanaa Tanzania – BASATA limefungia wimbo mpya wa mkali wa Bongo Fleva, Nay wa mitego unaoitwa, ‘ Shika adabu yako’. BASATA wamefikia uamuzi huo mgumu kwa kile walichodai kwamba ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na uchochezi. ”1: BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa…

NICK CANNON, STEVIE J NUSURA WAZICHAPE

  Supastaa wa Marekani mwenye vipaji lukuki, Nick Cannon,  amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutokea vita ya maneno dhidi yake na Stevie J. Ishu hiyo ilitokea mwanzoni mwa juma hili kwenye jukwaa la Mtv Base Rhyme lililopewa jina la Wild N’ Out ambapo Nick alikuwa aki-host shoo hiyo. Wawili hao walijukuta wakiingia katika malumbano baada ya…

BEBE COOL AVUTA MKOKO WA BEI MBAYA

Mwanamuziki mashuhuri wa Uganda, Moses Sali,  maarufu kwa jina la steji ‘Bebe Cool’ ameamua kujipongeza kwa kununua mkoko(gari) wa bei mbaya. Nyota huyo ali-post picha ya gari lake jipya la kifahari aina ya ‘Mercedes Benz CLS  350′ kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram. ”Maisha ni vile unavyoyatengeneza, kama utasafiri salama, daima utafikia sehemu uliyokusudia”, aliandika Bebe.…

WILL SMITH AJIBU TUHUMA NZITO ZINAZOMKABILI MTOTO WAKE WA KIUME

Mkongwe wa filamu kutoka hollywood Marekani, Will Smith hatimaye amefunguka kuhusiana na kashifa za uvaaji wa mavazi ya kike zinazomwandama mtoto wake wa kiume aitwaye jaden. Akizungumza kwenye mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha BBC1, Will alinukuliwa akisema ‘Jaden’ amekuwa akiamini  kile anachokifanya katika sanaa yake ya mitindo licha kwa upande wao kama wazazi imekuwa ikiwaogopesha. ”Asilimia 100 Jaden…

JUSTIN BIEBER AYAANIKA MAKALIO YAKE MTANDAONI

Mwanamuziki nyota wa marekani, Justin Bieber, ame-break the internet kwa style ya aina yake kufuatia picha tata aliyopost mtandaoni. Bieber ali-post picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa mtupu kama alivyozaliwa na kupelekea kuonyesha sehemu zake nyeti ikiwemo makalio. ”Look”, ali-add caption JB.  

MCHUMBA WA KARAMA ‘BELA’ AMTOLEA UVIVU INSPECTOR HARUNI

Mchumba wa muda mrefu wa memba wa kundi la Gangwe Mobb, Luteni Karama, Isabela Mpanda A.K.A Bella, amemtolea uvivu shemeji yake, Haruna Kaena ‘Inspector Haruni kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram. Akijinasibu pasipo kupepesa, Bela amefunguka kwamba, Inspector Haruni, amekuwa akimsingizia kuwa amekuwa akimkataza  Karama kupiga show za kundi lao na hivyo kujikuta akichukua mkwanja…

DIAMOND AMPIGIA SALUTI A.Y

Diamond Platnumz amemmwagia sifa kemkem mwanamuziki mwenzake, Ambwene Yessayah A.K.A A.Y ambaye alikuwa akisherekea  siku yake ya kuzaliwa wikiendi iliyopita (Julai,05) . Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook, Diamond alianza kwa kumpongeza mwanamuziki huyo kwa kuweza kuwajengea daraja la kimataifa na kuongeza kuwa  ndiye aliyefanikisha collabo yake ya kwanza kimataifa na mwanamuziki wa Nigeria, Davido,…

VIDEO YA DAVIDO ‘FANS MI’ MATATANI

Kwa mujibu wa gazeti la Nigeria, New Telegraph, Supastaa wa miondoko ya Afrobeats, Davido,yupo chini ya uchunguzi na Chombo cha Taifa cha udhibiti wa dawa za kulevya nchini humo kinachojulikana kama National Drug Law Enforcement Agency(NDLEA). Uchunguzi huo unakuja kufuatia video mpya ya msanii hiyo inayoitwa ‘Fans Mi’ ambayo amemshirikisha Rapa wa Marekani, Meek Mill,…

KTMA 2015 : ORODHA YA MAJINA YA WASHINDI WALIOTWAA TUZO ZA KILI

Usiku wa jana ulikuwa wa aina yake baada ya kufanyika sherehe za utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Music  ambapo wasanii wanaofanya muziki wa aina mbalimbali kama vile Hip Hop, Bongo Fleva, Dansi pamoja na Taarab waliweza kushindanishwa katika vipengele 33 vilivyokuwa vinawaniwa.  Katika utoaji wa Tuzo hizo, Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba aliweza kung’aa…

KIM KARDASHIAN AMUANGUSHIA KANYE WEST BONGE LA BIRHDAY

Mwanamitindo nyota na star wa kipindi cha televisheni cha KEEPING UP WITH THE KARDASHIANs, Kim K, amemdondoshea bonge moja la birthday baba wa mtoto wake, Kanye West wakati alipokuwa akisherekea kutimiza umri wa miaka 38. Inaelezwa kwamba Kim Kardashian aliteketeza takribani dola 110,000 kukodisha uwanja mkubwa wa basketball wa Staples Center ambapo Kanye West na…

PIGO BONGO MOVIES : MZEE KANKAA AFARIKI DUNIA

Msanii mkongwe wa maigizo na filamu  Bongo, Mzee Kankaa, amefariki Dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu. Mzee Kankaa alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya 2008 kupitia igizo la JUMBA LA DHAHABU lililokuwa likirushwa hewani na kituo cha TBC1 chini ya kiongozi wao Tuesday Kihangala. Mazishi yake ni leo hii majira ya saa 10…