JERRY MURO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Mkuu wa Idara ya habari  na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amefiwa na baba yake mzazi, mzee Cornel Muro usiku wa kuamkia leo. Kifo cha baba Mzazi wa Muro kimetokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hapo jana mishale ya saa 3 usiku baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu saratani ya koo la chakula. Kwa…

MGOMBEA MWENZA : JOHN POMBE MAGUFULI MGOMBEA URAIS C.C.M 2015

 Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Biharamulo Mashariki kupitia tiketi ya C.C.M, John Pombe magufuli amechaguliwa kuwania kiti cha urais C.C.M Bara. Uteuzi huo umekuja kufuatia mchujo wa makada wa tano waliopitishwa na kamati kuu ya maadili ukiongozwa na mwenyekiti wa C.C.M taifa, Dkt Jakaya mrisho Kikwete na kupatikana watatu waliochaguliwa na halmashauri kuu ya…

MBUNGE JOSHUA NASSARI WA ARUMERU MASHARIKI ANUSURIKA KATIKA AJALI YA CHOPA

Mbunge wa Jimbo la Arumeri Mashariki, Joshua Nassari amepata ajali ya Helkopta aliyokuwa akiitumia kufanya ziara jimboni kwake hii leo. Habari kutoka Arumeru zinasema kuwa Helkopta hiyo ilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga mti na kunasa juu ya mti huo. Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo kwa Tiketi ya Chadema, na rubani wake walitoka wakiwa…

SAKATA LA GWAJIMA : MAASKOFU KUKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA

  Maaskofu kutoka madhehebu mbali mbali ya Kikristo nchini Tanzania wanakusudia kuonana na mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu, ili kupata suluhu kuhusu sakata linalomkabili mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, askofu Josephat Gwajima. Aidha, maaskofu hao pia wameonyesha masikitiko ya kile walichodai kuwa ni vituo vya polisi kutoonekana kuwa ni mahali…

WAGANGA WA KIENYEJI WAWACHIMBA MKWARA POLISI

Wakati msako wa kuwakamata waganga wapiga ramli chonganishi ukiendelea nchi nzima hasa katika mikoa ya kanda ziwa, jeshi la polisi nchini limepewa onyo toka kwa wanganga wa jadi juu ya vifaa vinavyokamatwa wakati wa msako wao. Jeshi hilo limepewa tahadhali ya kukumbana na hatari yeyote baadaye ikiwa wataendelea kukamata vifaa hivyo vikiwamo vibuyu, vitambaa vyeupe…

ZITTO KABWE ATANGAZA RASMI KUACHIA UBUNGE

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya CHADEMA, Zitto Zuberi Kabwe, amewaaga rasmi wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jioni ya leo mara baada ya kumalizika kwa shughuli za Bunge. Aidha Mbunge huyo ametangaza rasmi kuachia nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kufuatia mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, kutangaza katika vyombo…

UPASUAJI WA KWANZA DUNIANI WA UPANDIKIZAJI UUME WAFANIKIWA

Jopo la Madaktari Afrika Kusini wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza Duniani wa kupandikiza uume kwa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 21 ambaye alipoteza kiungo chake hicho baada ya kufanyiwa tohara vibaya.  Ingawa upasuaji wa namna kama hiyo umewahi kufanyika awali, ila huu unatajwa kuwa upasuaji wa kwanza ambao mtu ameweza kupona na kiungo hicho…

ALICHOKISEMA MWIGULU NCHEMBA BAADA YA ZITTO KABWE KUVULIWA UANACHAMA CHADEMA

Naibu waziri wa fedha  ‘Mwigulu Nchemba’ ameonyesha kusikitishwa na uamuzi uliotolewa na Chama cha demokrasia na Maendeleo kupitia mwanasheria wake Tundu Lissu kufuatia kumvua uanachama mbunge wa Kigoma Kaskazini, mheshimiwa Zitto Kabwe hapo jana. ”IMENISIKITISHA,Nimesikia taarifa za kuenguliwa uanachama kwa Mh.Zitto Kabwe ndani ya Chama alichoanzia siasa,alichokitumikia kwa Jasho na mali,alichowekeza muda na akili yake…

AJALI MBAYA YA BASI NA LORI YAUA WATU 42 MKOANI IRINGA

AJALI mbaya ya gari imetokea asubuhi ya jana saa 3.30 Jumatano katika kijiji cha Changarawe wilayani Mufindi mkoani Iringa baada ya basi la abiria la kampuni iitwayo Majinja lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, kugongana na lori la mizigo lililokuwa likitokea Dar kuelekea Mbeya na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kufikia 42 na majeruhi…

PICHA : RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA STUDIO MPYA ZA AZAM TV

Rais Jakaya Kikwete amezindua studio mpya za kisasa zaidi kuliko zote Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazomilikiwa na Azam TV jijini Dar es salaam hapo  jana(Mar.06). Katika uzinduzi huo naibu Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, ndg Tido Mhando, amesema wazo la kuanzishwa kwa Azam TV lilitoka Azam FC.  Tazama picha zaidi hapo chini.     …

ALBINO WAZICHAPA KAVUKAVU IKULU

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wamepigana ngumi na mateke wakigombea kuingia kumwona Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ambapo lilianzia kwenye eneo la mapokezi Ikulu mara baada ya walemavu hao kukaguliwa na kuwekwa kwenye chumba…

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA KAPTENI JOHN KOMBA MBEZI BEACH TANGI BOVU JIJINI DAR

Rais Jakaya Kikwete ameungana na waombolezaji wengine kuitembelea familia ya aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Marehemu Kapteni John Komba aliyefariki Dunia katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam hapo jana. Akitokea Dodoma akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na mkewe  Mama Salma kikwete, Rais Kikwete ametia saini kitabu cha maombolezo na…

UBUNIFU KUTOKA MOYONI : AUNDA NDEGE KWA KUTUMIA MISOKOTO YA BANGI

Ukisikia ubunifu kutoka moyoni ndio huu. Wakati baadhi ya nchi za magharibi zikihalalisha uvutaji wa bangi, fursa hiyo imeonekana kuwapa nafasi watu flani kuonyesha ujuzi wao wa kuunda mmea huo ambao unapigwa vita vikali barani Afrika na kwingineko. Katika pitapita zangu mitandaoni, nikabahatika kukutana na jamaa mmoja ambaye aliamua kutumia misokoto ya bangi na kuunda …