NGOMA MPYA : LEE CHATTO – WANAPAGAWA

Mwanamuziki chupikizi wa Bongo Fleva, Ally Chatto A.K.A Lee Chatto ambaye ameonyesha kuwa na kipaji cha hali ya juu katika kuchana licha ya umri wake mdogo. Ameachia ngoma yake ya kwanza inayoitwa “Wanapagawa” ambayo imefanywa kwenye studio za Sound Special chini ya Producer Tytah. Isikilize na kuipakua hapa      

NGOMA MPYA : RONY – MABEBE

Msanii wa muziki wa kizazi  kipya ‘Rony’ ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mabebe ambayo imefanywa kwenye studio ya Skeleton Music Production chini ya Producer S2keys. Isikilize na kuipakua hapo chini 

BLAC CHYNA KATIKA MUONEKANO WA KIBANTU

Supastaa na mzazi wa Rapa Tyga, Blac chyna, ametupia baadhi ya picha kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram zikimuonyesha akiwa amesuka mtindo wa kibantu ambao hutumiwa sana na wanawake wengi wa ki-Afrika. Kama hiyo haitoshi staa huyo alitumia mwanya huo kuwaonyesha mashabiki wake pete ya uchumba aliyovishwa na mdogo wa kiume wa Kim Kardshian aitwaye…

50 CENT AMDISS P.DIDY

Rapa 50 cent amekuwa akisifika kwa kupenda ma-bifu na wasanii wenzake ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakipelekea uhasama baina yao. Safari hii hitmaker huyo wa In Da Club, amemdiss mmilikiwa studio za bad Boys, Sean Combs A.K.A P.Diddy kwa kumwambia kuwa hana sifa za kuitwa msanii. Akichezesha taya kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Dj Enuff, 50 Cent…

PICHA : BIRTHDAY YA MIAKA 2 YA EFM 93.7 NDANI YA MAISHA BASEMENT

  Kituo maarufu mjini cha utangazaji, Efm, kinachopatikana kwenye masafa ya 93.7 jijini Dar es salaam, mwanzoni mwa juma hili(Jumatatu) waliangusha bonge la birthday katika kusherekea kutimiza miaka 2 tangu kuzaliwa kwake ndani ya ukumbi wa burudani wa maisha Basement. Wahenga wanakwambia mwenye macho haambiwi tazama, nisikuchoshe sana fanya kutazama hapo chini ujionee mambo yalivyokuwa.…

TAZAMA MUONEKANO MPYA WA JUSTIN BIEBER

Supastaa daraja la kwanza asiyehishiwa vituko kila kukicha, Justin Bieber, amewa-suprise mashabiki wake kwa kutokelezea na mtindo mpya wa nywele. Muimbaji huyo Raia wa Canada aliwashangaza mashabiki wake wakati alipokuwa aki-perform kwenye sherehe za utoaji Tuzo za iHeartRadio akiwa amesokota nywele zake(Dreadrocks) na kumfanya kuwa kivutio kikubwa jukwaani. katika Tuzo hizo, Bieber alifanikiwa kunyakuwa Tuzo…

BASATA WAFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO ‘SHIKA ADABU YAKO’

Baraza la Sanaa Tanzania – BASATA limefungia wimbo mpya wa mkali wa Bongo Fleva, Nay wa mitego unaoitwa, ‘ Shika adabu yako’. BASATA wamefikia uamuzi huo mgumu kwa kile walichodai kwamba ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na uchochezi. ”1: BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa…

NICK CANNON, STEVIE J NUSURA WAZICHAPE

  Supastaa wa Marekani mwenye vipaji lukuki, Nick Cannon,  amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutokea vita ya maneno dhidi yake na Stevie J. Ishu hiyo ilitokea mwanzoni mwa juma hili kwenye jukwaa la Mtv Base Rhyme lililopewa jina la Wild N’ Out ambapo Nick alikuwa aki-host shoo hiyo. Wawili hao walijukuta wakiingia katika malumbano baada ya…

BEBE COOL AVUTA MKOKO WA BEI MBAYA

Mwanamuziki mashuhuri wa Uganda, Moses Sali,  maarufu kwa jina la steji ‘Bebe Cool’ ameamua kujipongeza kwa kununua mkoko(gari) wa bei mbaya. Nyota huyo ali-post picha ya gari lake jipya la kifahari aina ya ‘Mercedes Benz CLS  350′ kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram. ”Maisha ni vile unavyoyatengeneza, kama utasafiri salama, daima utafikia sehemu uliyokusudia”, aliandika Bebe.…

WILL SMITH AJIBU TUHUMA NZITO ZINAZOMKABILI MTOTO WAKE WA KIUME

Mkongwe wa filamu kutoka hollywood Marekani, Will Smith hatimaye amefunguka kuhusiana na kashifa za uvaaji wa mavazi ya kike zinazomwandama mtoto wake wa kiume aitwaye jaden. Akizungumza kwenye mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha BBC1, Will alinukuliwa akisema ‘Jaden’ amekuwa akiamini  kile anachokifanya katika sanaa yake ya mitindo licha kwa upande wao kama wazazi imekuwa ikiwaogopesha. ”Asilimia 100 Jaden…

ANDY MURRAY APATA MTOTO WA KIKE

Mchezaji nyota wa mchezo wa tenesi Duniani, Andy Murray na mkewe ‘Kim Sears’ wamebahatika kupata mtoto wao wa kwanza wa kike wikiendi iliyopita. Hata hivyo jina la mtoto huyo alikuweza kufahamika mara moja huku taarifa rasmi kutoka kwenye familia ya wanandoa hao ikisubiriwa. Mashabiki na wadau mbalimbali wa michezo Duniani wameweza kumpongeza nyota huyo kwenye mitandao…