HAJI MANARA : TFF NA BODI YA LIGI WANAANDAA MAZINGIRA KUWASAIDIA YANGA KUPATA UBINGWA

Haji Manara

Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema hakuna kificho juu ya mipango ya kutaka timu flani iwe bingwa wa ligi kuu msimu huu hasa kutokana na mabadiliko ya mara kwa  mara ya ratiba ya ligi hiyo.

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo ‘Haji Manara’ amesema wanashangazwa kuona mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe hii leo ukisogezwa hadi April 16 mwaka huu.

Wakati siku mbili baadae Yanga itatakiwa kuwa nchini Misri kurudiana na Al-Ahly hivyo ni wazi hata mchezo huo wa Tarehe 16 nao utasogezwa mbele na Yanga kuzidi kuwa na viporo.

Lakini unapanga ratiba wacheze tarehe 16 Dar es salaam na Mtibwa hiyohiyo alafu baada ya siku 3 wacheze Cairo, hapa kuna mchezo unatengenezwa, kuna kitu wanakifiksi, what next? Mnakijua? Ni nini? Mechi ya Tarehe 16 imepangwa kuahirishwa tena, yaani hiyo wanacheza shere’’, alisema Haji Manara.

Aliongeza : ‘’Yanga haohao wakatae kucheza leo ili wajiandae Jumamosi, alafu wakubali kucheza Tarehe 16 Dar es salaam, wacheze Cairo Tarehe 19, Simba sio wajinga, tunajua na tunaamini TFF na bodi ya Ligi wanaandaa mazingira sasa ya kuwasaidi yanga kupata ubingwa’’.

Kwa upande mwingine Manara amesema kufuatia kipa wao aliye kwa mkopo kwa timu ya Geita kufungiwa za upangaji matokeo za mechi ya ligi daraja la kwanza kundi C, wameitaka Takukuru kwenda kukita kambi TFF ili kupata watuhumiwa zaidi kutokana na taarifa zilizoenea nchini ya kwamba baadhi ya viongozi wa juu wa TFF wanahusika na sakata hilo.

’Kwa tuhuma tulizozisikia jana, tunaiomba TAKUKURU ikapige kambi TFF pale kuna zaidi ya kilichoamuliwa, mchezaji wetu hatusemi ameonewa, tunaiomba TAKUKURU mamlaka husika inayosimamia upigaji vita rushwa ikapigwe camp pale, uchunguzi wake uanzie juu kabisa’’.

Chanzo : EATV

Advertisements

One thought on “HAJI MANARA : TFF NA BODI YA LIGI WANAANDAA MAZINGIRA KUWASAIDIA YANGA KUPATA UBINGWA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s