NICK CANNON, STEVIE J NUSURA WAZICHAPE

 

Supastaa wa Marekani mwenye vipaji lukuki, Nick Cannon,  amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutokea vita ya maneno dhidi yake na Stevie J.

Nick mariah carey stevie j

Nick Cannon, Mariah Carey, Stevie J

Ishu hiyo ilitokea mwanzoni mwa juma hili kwenye jukwaa la Mtv Base Rhyme lililopewa jina la Wild N’ Out ambapo Nick alikuwa aki-host shoo hiyo.

Wawili hao walijukuta wakiingia katika malumbano baada ya kila mmoja kumponda mwenzake kuhusiana na wapenzi wao wa zamani kufuatia Cannon kumtusi mpenzi wa Stevie J, Josephine Hernandez, aliyekuwa ameambatana nae kwamba amekuwa akimsaliti kwa kutoka na Rapa Rick Ross.

Stevie J Nick Cannon Josephine Hernandez

Stevie J aliyevaa Pama akishuhudiwa na mpenzi wake Josephine(Wa kwanza kushoto)  wakati akimtambia Nick Cannon aliyeshika kipaza sauti

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Reality Star wa Love & Hip hop Atlanta ‘Stevie J’ kujibu mashambulizi kwa kutamba kuwa amekwisha vunja amri ya sita mara mbili  na mama watoto wakeMariah Careykipindi hicho akiwa producer wake aliyemtengenezea kibao cha Honey kilichotokea kubamba kwenye albamu yake ya Butterfly iliyotoka 1997.

Ubishani huo ulimalizika kwa Nick Cannon kumwambia Stevie J kwamba hatofanya tena kazi katika jiji la Hollywood ambapo mashuhuda walidai kwamba kama ubishani huo ungeendelea basi mastaa hao wangeweza kuzichapa hadharani.

Nick na Mariah walifunga ndoa March 30, 2008 na kubahatika kupata watoto 2 mapacha Monroe na morrocan mwaka 2011 kabla ya ndoa  yao kuvunjika August 2014 na kila mtu kuchukua hamsini zake.

Kwa sasa Mariah Carey yupo kwenye mahusiano na bilionea wa Australia, James Parker, ambaye alitangaza rasmi kuvishwa pete ya uchumba Jan.21 mwaka huu.

Mariah Carey James Parker

Mariah Carey na James Parker katika pozi

Nick and Mariah Wedding

Mariah Carey na Nick Cannon siku ya ndoa yao

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s