BASATA WAFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO ‘SHIKA ADABU YAKO’

Nay Wa Mitego - Mr. Nay

Baraza la Sanaa Tanzania – BASATA limefungia wimbo mpya wa mkali wa Bongo Fleva, Nay wa mitego unaoitwa, ‘ Shika adabu yako’.

BASATA wamefikia uamuzi huo mgumu kwa kile walichodai kwamba ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na uchochezi.

”1: BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, uchochez”, waliandika BASATA kwenye ukurasa wao wa twitter

Hawakuishia hapo walienda mbele zaidi kwa kumpa karipio kali msanii huyo na kumtaka aache kuutangaza wimbo huo katika media vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia wameweka wazi kuwa hata sheria kifungu cha 4(1)(j) & 4(2) cha sheria ya BASATA kinalipa Baraza mamlaka ya kuratibu/kufuatilia miendendo ya mtu yeyote anayehusika na Sanaa huku vikilipa nguvu baraza hilo kulinda maadili ya kitaifa na kufanya jambo lolote lile katika sanaa kwa faida na ustawi wa taifa.

Mwisho kabisa baraza hilo limetoa onyo ya kutowavumilia baadhi ya wasanii wachache wanaotaka kuigeuza tasnia ya sanaa kuwa genge la wahuni wasio na staha

Tazama baadhi ya tweets walizoandika BASATA kuhusiana na wimbo huo

BASATA1

BASATA2

 

 

Advertisements

2 thoughts on “BASATA WAFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO ‘SHIKA ADABU YAKO’

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s