WILL SMITH AJIBU TUHUMA NZITO ZINAZOMKABILI MTOTO WAKE WA KIUME

Will & Jaden

Mkongwe wa filamu kutoka hollywood Marekani, Will Smith hatimaye amefunguka kuhusiana na kashifa za uvaaji wa mavazi ya kike zinazomwandama mtoto wake wa kiume aitwaye jaden.

Akizungumza kwenye mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha BBC1, Will alinukuliwa akisema ‘Jaden’ amekuwa akiamini  kile anachokifanya katika sanaa yake ya mitindo licha kwa upande wao kama wazazi imekuwa ikiwaogopesha.

”Asilimia 100 Jaden sio muoga,  yeye anaweza akafanya kitu chochote, tukiwa kama wazazi inatutisha, kweli inatishia.  Lakini yeye yupo tayari kuishi  na kufa kwa maamuzi yake mwenyewe kisanii, wala hajali watu wanamchukuliaje”, alisema Will

Aliongeza :Unaweza  ukawa unajaribu vitu na kupenda kuendelea kuvifanya ambavyo jamii haikubaliani nayo, na unaweza ukawa huru  kufanya vitu ambavyo unaweza ukavishindwa”.

Hatua hiyo imekuja kufuatia vyombo mbalimbali vinavyoandika habari hasa za udaku kummulika staa huyo wa The Karate Kid ambaye amekuwa akijihusisha na mitindo huku mavazi anayoyatumia kwenye sanaa yake yakipelekea jamii kumfikiria ndivyo sivyo.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s