MCHUMBA WA KARAMA ‘BELA’ AMTOLEA UVIVU INSPECTOR HARUNI

Isabela Mpanda 'Bella' akionyesha pete ya uchumba aliyovishwa na laaziz wake 'karama' kushoto aliyevaa miwani meusi miezi michache iliyopita

Isabela Mpanda ‘Bella’ akionyesha pete ya uchumba aliyovishwa na laaziz wake ‘karama’ kushoto aliyevaa miwani meusi miezi michache iliyopita

Mchumba wa muda mrefu wa memba wa kundi la Gangwe Mobb, Luteni Karama, Isabela Mpanda A.K.A Bella, amemtolea uvivu shemeji yake, Haruna Kaena ‘Inspector Haruni kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.

Akijinasibu pasipo kupepesa, Bela amefunguka kwamba, Inspector Haruni, amekuwa akimsingizia kuwa amekuwa akimkataza  Karama kupiga show za kundi lao na hivyo kujikuta akichukua mkwanja wote kwa kutumia kisingizio hicho.

ʽʽhuuu sasa nikama mwaka wa kumi. kila ukienda sehem au show lazima uniuwe mimi oooh bela anamkataza @lutenkarama asifanye kazi oooh bela atak karama awe na washkaji . na mda mwingine usha sema uwongo dar live @globalpublishers kuwa karama hatak hii show pesa zote nipewe mimi ila walitumia akili ilipo fika saa 5 usiku uwongoz wa @globalpublishers walimpigia sim karama na kumuuliza why hutak show eti bela anakukataza kufanya showˮ, aliandika Bella

Aliongeza kuwa siyo chini ya watu 40 waliokuwa wakitaka wakali hao wa kitambo ‘Gangwe Mobb’ kupiga show lakini Inspector amekuwa akikimbilia kusema kwamba Karama awezi kuja kisa amebanwa na mpenzi wake na kwenda mwenyewe kupiga show na kuchukua hela ya kundi.

ʽʽkuna watu wengi siyo chin ya 40 kazi yake zikija show za kundi yeye ana kimbilia karama awez kuja dem kambana dem atak afanye kaz. au ana chukua pesa ya kundi akifika siku ya show anaenda peke yake akiulizwa mbona umekuja mwenyewe anajibu karama kagoma kuamka kisa bela anamkatazaˮ.

Pia alidai kuna siku Global Publishers walishtukia mchezo baada ya show waliyotakiwa kupiga kama kundi katika kiota cha burudani ‘Dar Live Mbagala’ lakini katika hali ya sintofahamu alitokea Inspector mwenyewe na kutaka pesa zote apewe yeye, hali iliyopelekea waandaaji wa show hiyo kupigia simu karama na kumkatia chake ambapo Karama alishangazwa na kudai hajui chochote kuhusu show.

ʽʽmda mwingine usha sema uwongo dar live @globalpublishers kuwa karama hatak hii show pesa zote nipewe mimi ila walitumia akili ilipo fika saa 5 usiku uwongoz wa @globalpublishers walimpigia sim karama na kumuuliza why hutak show eti bela anakukataza kufanya show . karama akashangaa na akawajibu ajui chochote kuhusu showˮ, alifunguka Bela.

Mpenzi huyo wa Karama ambaye pia ni mwanamuziki wa kundi la Scorpion Girls, amewataka mashabiki waelewe kwamba hamkatazi Karama kufanya kazi yeyote ile na kupiga marufuku Inspector kutaja jina lake na kudai kuwa hata wasanii wenzake wakubwa wamemchoka na mambo ambayo amekuwa akimfanyia Karama.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s