VIDEO YA DAVIDO ‘FANS MI’ MATATANI

Davido na Meek Mill MMG Kwa mujibu wa gazeti la Nigeria, New Telegraph, Supastaa wa miondoko ya Afrobeats, Davido,yupo chini ya uchunguzi na Chombo cha Taifa cha udhibiti wa dawa za kulevya nchini humo kinachojulikana kama National Drug Law Enforcement Agency(NDLEA).

Uchunguzi huo unakuja kufuatia video mpya ya msanii hiyo inayoitwa ‘Fans Mi’ ambayo amemshirikisha Rapa wa Marekani, Meek Mill, kuonyesha  vitu vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.

Wimbo wa Fans Mi ulikuwa na lengo la Kuwashukuru mashabiki kwa mapenzi na ushirikiano waliomuonyesha Davido katika kipindi chote tangu ajikite katika gemu la muziki.

Hata hivyo video ya muziki huo inaonekana kuwazungumzia zaidi maadui na fedha za mwanamuziki huyo.  Pia video hiyo inaonyesha madawa ya kulevya, wanawake waliovaa nusu utupu pamoja na silaha za moto.

Huku moja ya kipande cha video hicho kikimuonyesha Davido akizungumza na jamaa mmoja na kisha kubadilishana mabegi ya fedha kwa madawa ya kulevya.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la telegraph linalotoka kila jumapili, Mkuu wa masuala ya Umma, Bw.Mitchell Ofeyeju, alinukulikuwa akisema kuwa video hiyo imekosa maadili na ni chafu.

Chombo chetu kimeichukulia video ya Fans Mi kukosa maadili na chafu”, alisema Ofeyeju

Aliongeza : “Pia inashawishi uvutaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya , mbali na hilo, ni kukabiliana na uzalishaji juu ya kampeni dhidi ya uzalishaji wa madawa ya kulevya, biashara haramu na unyanyasaji”.

Alihitimisha kwa kusema kuwa chombo hicho kinachunguza suala hilo na kitachukua hatua muhimu. 

Mpaka sasa Video ya Fans Mi imefikisha jumla ya watazamaji milioni 1 na laki 3 kwenye mtandao wa Youtube.  Itupie jicho hapo chini

[youtube  https://www.youtube.com/watch?v=3E6pwUO1b7s&w=620&h=415%5D

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s