NDUGU ZANGU WA WHATSAPP NIPUNGUZIENI MSG KIDOGO MTANIULIA KISIMU CHANGU – DIAMOND

Diamond PlatnumzMwanamuziki daraja la kwanza wa muziki wa Bongo Fleva hapa Bongo, Diamond Platnumz amewaomba mashabiki zake wapunguze hasira za kumtumia meseji kwenye mtandao wa Whatsapp maana wakiendelea hivyo huenda wakamuulia simu yake.

Diamond amefikia hatua hiyo baada ya kuona akitumiwa meseji nyingi kwenye mtandao huo na hivyo kulazimika ku-Screenshot simu yake ambayo ilikuwa ikionyesha   jumla ya meseji 10,582 alizotumiwa kwa wakati huo na kisha ku-post kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.

Ndugu zangu wa WhatsApp walau nipunguzieni punguzieni Msg kidogo, Mtaniulia kisimu changu cha Ngama jamani…😭”, aliandika Diamond .

Kauli hiyo ya Diamond inakuja ikiwa ni miezi minne kupita tangu blog ya Larrybway91 ilipomgongea hodi mjengoni kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya mahojiano lakini katikati ya mazungumzo alituambia kuwa inafika kipindi anashindwa kujibu meseji kwenye mtandao huo kutokana na jam kubwa ya watu wanaomtumia.

Huwa sipokeagi simu, maana huwezi kuamini, kwa siku naweza kupokea text zaidi ya elfu mbili kupitia Whatsapp, ndio maana inakuwa ni vigumu kujibu meseji za watu kwa haraka”, Diamond aliiambia Blog ya Larrybway91 baada ya kutwangwa swali la kizushi kuhusiana kutopenda kupokea simu mara kwa mara.

Diamond ScreenShot

Mpenzi msomaji unaweza ukatazama screenshot aliyopost ‘Diamond’ ikionyesha idadi ya meseji alizotumiwa Whatsapp

 

 

Advertisements

One thought on “NDUGU ZANGU WA WHATSAPP NIPUNGUZIENI MSG KIDOGO MTANIULIA KISIMU CHANGU – DIAMOND

  1. Nakushauri .hatakama ulishea nae mapenzi uskatae mimba ,ila usikubari kubambikwa mtoto kapime dnme .na kipimo kikionyesha sio wako basi mtoto atakuwa ana baba mtunze utazidishiwa na mungu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s