SAKATA LA GWAJIMA : MAASKOFU KUKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA

 

Baadhi ya Maaskofu wakifuatilia kwa makini tamko lililokuwa linatolewa na wenzao ambao hawapo pichani.

Baadhi ya Maaskofu wakifuatilia kwa makini tamko lililokuwa linatolewa na wenzao ambao hawapo pichani.

Maaskofu kutoka madhehebu mbali mbali ya Kikristo nchini Tanzania wanakusudia kuonana na mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu, ili kupata suluhu kuhusu sakata linalomkabili mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, askofu Josephat Gwajima.

Aidha, maaskofu hao pia wameonyesha masikitiko ya kile walichodai kuwa ni vituo vya polisi kutoonekana kuwa ni mahali salama kwa watuhumiwa wa makosa mbali mbali wanaofikishwa hapo.


Askofu Gwajima amelazwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alikopelekwa kwa matibabu baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akihojiwa na polisi, kwa tuhuma za kumkashifu askofu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam, Muadhama Kadinali Polycarp Pengo.  Habari na Picha kwa hisani ya EATV

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s