ZITTO KABWE ATANGAZA RASMI KUACHIA UBUNGE

Zitto KabweMbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya CHADEMA, Zitto Zuberi Kabwe, amewaaga rasmi wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jioni ya leo mara baada ya kumalizika kwa shughuli za Bunge.

Aidha Mbunge huyo ametangaza rasmi kuachia nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kufuatia mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, kutangaza katika vyombo vya habari kumfuta uanachama mbunge huyo kutokana na kukishtaki chama hicho.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ninaomba kukutaarifu wewe na Bunge lako tukufu kwamba sina mpango wa kuendelea kupigania uanachama wangu wa CHADEMA katika viunga vya mahakama”. Alisema Kabwe

Kwa hiyo ninatangaza rasmi leo kwamba taratibu za kikatiba zitakapokamilika tu nitaachia uanachama wa CHADEMA, chama nilichokipenda sana kwa sababu ya kuendelea kukua kwa tofauti za kiitikadi, kimtazamo na hata kibinafsi kati yangu na viongozi katika chama changu‘, aliongeza Zitto

Nimeona kuwa kuendelea kupigania uanachama kisheria ni kutatiza na kukwaza harakati za mabadiliko hapa nchini katika wakati ambapo mfumo wa kisiasa unatambua uwepo wa vyama vingi vya siasaKwa kuwa taratibu hizo sijui zitakamilika lini, natumia fursa hii kuwaaga wabunge wenzangu kuwashukuru kwa ushirikiano na kumalizia kwa kusema kuwa  “MUNGU AKIPENDA TUTAKUWA WOTE MWEZI NOVEMBA” .”

 

 

Advertisements

One thought on “ZITTO KABWE ATANGAZA RASMI KUACHIA UBUNGE

  1. Usaliti mbaya sana alipewa tuhuma akahepa sasa yamemkuta nenda ukalime kwenu na chama chako cha ACT

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s