UPASUAJI WA KWANZA DUNIANI WA UPANDIKIZAJI UUME WAFANIKIWA

MadaktraiJopo la Madaktari Afrika Kusini wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza Duniani wa kupandikiza uume kwa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 21 ambaye alipoteza kiungo chake hicho baada ya kufanyiwa tohara vibaya. 

Ingawa upasuaji wa namna kama hiyo umewahi kufanyika awali, ila huu unatajwa kuwa upasuaji wa kwanza ambao mtu ameweza kupona na kiungo hicho kuweza kufanya kazi ipasavyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na chuo kikuu cha Stellenbosch kwa vyombo vya habari, Zoezi hilo la upasuaji  lilidumu kwa takribani saa 9 likiongozwa na Dokta Andre Van der Merwe kwenye hospitali ya Tygerberg mjini Cape town mwezi Desemba mwaka jana.

Baada ya miezi mitatu kupita, chuo hicho kilitangaza  kuwa mgonjwa huyo  amepona na kiungo chake kimeweza kufanya kazi vizuri.

Lengo letu ni kwamba kiungo hicho kingepaswa kufanya kazi kwa miaka miwili, sisi tumeshangazwa sana na ahueni yake ya haraka, alisema Van Der Merwe katika vyombo vya habari ”Matokeo ya mwisho ya kupandikiza ilikuwa marejesho ya mkojo na ufanyaji kazi wa viungo vya uzazi”.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s