ALICHOKISEMA MWIGULU NCHEMBA BAADA YA ZITTO KABWE KUVULIWA UANACHAMA CHADEMA

Mwigulu Nchemba na Zitto KabweNaibu waziri wa fedha  ‘Mwigulu Nchemba’ ameonyesha kusikitishwa na uamuzi uliotolewa na Chama cha demokrasia na Maendeleo kupitia mwanasheria wake Tundu Lissu kufuatia kumvua uanachama mbunge wa Kigoma Kaskazini, mheshimiwa Zitto Kabwe hapo jana.

IMENISIKITISHA,Nimesikia taarifa za kuenguliwa uanachama kwa Mh.Zitto Kabwe ndani ya Chama alichoanzia siasa,alichokitumikia kwa Jasho na mali,alichowekeza muda na akili yake kwa zaidi ya miaka 19”, aliandika Nchemba kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuongeza, ”Zitto amekuwa/anaendelea kuwachachu ya mabadiliko kwa Vitendo kwa Taifa letu.Uwezo wa kisiasa wa Kabwe adhabu yake sio kumfukuza,Demokrasia ni lazima itumike”.

Aidha mbunge huyo wa Iramba magharibi kupitia tiketi ya CCM amemsihi mheshimiwa Zitto kutokukataa tamaa na kamwe watanzania hawatoweza kusahau mema aliyoyafanya kwa ajili ya manufaa ya taifa hili.

Nakusihi kijana Mwenzangu,Mwanasiasa Mwenzangu na Mchumi Mwenzangu kuwa,Taifa linakuhitaji sana wakati huu tunapopambana na ufanyaji kazi kwa mazoea na kuleta “MABADILIKO KWA VITENDO”Hivyo usikate tamaa watanzania watakuhesabia mema kwa yote unayoyafanya kwaajili ya Taifa letu”.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s