RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA KAPTENI JOHN KOMBA MBEZI BEACH TANGI BOVU JIJINI DAR

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Kapteni John Komba aliyefariki jioni ya tarehe 28 februari 2015 jijini Dar es salaam,kushoto ni mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete.

Rais Jakaya Kikwete ameungana na waombolezaji wengine kuitembelea familia ya aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Marehemu Kapteni John Komba aliyefariki Dunia katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam hapo jana.

Akitokea Dodoma akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na mkewe  Mama Salma kikwete, Rais Kikwete ametia saini kitabu cha maombolezo na kisha kuzungumza na familia ya marehemu.

Spika wa bunge Anna Makinda amesema pengo la kiongozi huyo halitaweza kuzibika kutokana na ucheshi uliomfanya kupendwa na wabunge wengi zaidi na kuwataka wabunge kufanya kazi kwa neema ya Mungu.

Nae Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara, Mwigulu Mchemba, amesema kifo cha marehemu ni pigo kubwa kwa CCM na kuwataka wanaccm kuyaenzi mambo yote huku waziri mkuu Edward Lowasa nae akiwataka wanaccm na wananchi kwa ujumla kumuenzi.

Akielezea taratibu za maziko mtoto wa marehemu ,Gerrard Komba amesema marehemu anatarajia kuzikwa kijijini kwao Manda mkoani Ruvuma hapo kesho kutwa.

 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mke wa marehemu Kapteni John Komba nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mke wa marehemu Kapteni John Komba nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu

 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisaini kitabu cha maombolezo

Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye akisaini kitabu cha maombolezo

TOT

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombelezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombelezo kwenye msiba wa Kapteni John Komba.

Nape Nnauye1

Nape akizungumza na waandishi wa habari

Bernard membe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamillius Membe akisaini kitabu cha maombolezo

nape nnauye Fredrick Sumaye

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anna Makinda akisaini kitabu cha maombelezo ya msiba wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anna Makinda akisaini kitabu cha maombelezo ya msiba wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s