USELA WAMPONZA CHRIS BROWN, AKATALIWA KUINGIA CANADA, ALAZIMIKA KUVUNJA MATAMASHA YAKE

Chris brownMwanamuziki nyota wa Marekani, Chris Brown ameendelewa kuandamwa na gundu baada ya kukataliwa kuingia nchini Canada na kulazimika kukatisha matamasha yake.

Brown mwenye umri wa miaka 25, ali-tweet kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumanne(Feb.24) kuwa  amekataliwa kuingia Canada na kwamba matamasha yake yaliyokuwa yafanyike katika miji ya Montreal na Toronto yamefutwa.

Watu wangu wa Canada, serikali imenikatalia kuingia. Nitarudi majira haya ya joto na natumaini nitawaona mashabiki wangu wote wa Canada”, aliandika Chris Brown.

Msemaji wa Brown, Nicole Perna alithibitisha kuwa kitengo cha uhamiaji cha Canada kilimkatalia bosi wake kuingia nchini humo . 

Alisema Brown anaweza kuomba kurudi katika siku za baadaye na anampango wa kufanya hivyo.

Nae Msemaji wa huduma za mipaka ya Canada, Stephane Malepart amesema nchi yake imemzuia supastaa huyo kutokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na kuhusika katika shughuli za uhalifu.

Hii sio mara ya kwanza kwa Chris Brown kunyimwa kuingia katika nchi za watu, kwani mwaka 2010 msanii huyo alikataliwa kuingia nchini uingereza na kulazimishwa kuzikosa shoo zake nne. 

Serikali ya Uingereza ilisema kwamba imemkatalia msanii huyo kwa sababu ya rekodi yake ya nyuma ya makosa ya jinai.

Mwaka jana ‘Brown’  alifungwa jela kwa takribani miezi 3  kwa kukiuka majaribio yake baada ya kupatwa na hatia ya kushambulia nje ya hoteli mjini Washington mwaka uliopita, kama hiyo haitoshi alikuwa katika majaribio baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake Rihanna kabla ya utolewaji wa tuzo za Grammy mwaka 2009.  

Kwa picha rahisi utaweza kuona ni jinsi gani wingi wa matukio hayo ya jinai yanavyomgharimu  hitmaker huyo wa Loyal na kujikuta akipishana na mkwanja mrefu.  

Hili linaweza kutumika kama fundisho kwa wasanii wetu wa hapa nyumbani kwamba too much Ego will kill your talen.  Bad Lucky Bruh C.B. 

Advertisements

One thought on “USELA WAMPONZA CHRIS BROWN, AKATALIWA KUINGIA CANADA, ALAZIMIKA KUVUNJA MATAMASHA YAKE

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s