CHUCHU HANS : SIJAACHANA NA RAY

Ray na Chuchu HansMsanii nyota wa filamu hapa Bongo, Chuchu Hans amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na  tetesi zilizozagaa mitandaoni za kupigwa chini na mpenzi wake ambaye pia ni mwigizaji mwenzake, Vicent Kigosi ‘Ray’ ambapo kwa mara ya kwanza habari hizo zilianza kuvuma kutoka katika mtandao wa Instagram.

Akitiririka katika mahojiano aliyofanyiwa na Zamaradi Mketema katika kipindi cha Take One kupitia Clouds Tv, Chuchu amesema yeye na Ray bado ni wapenzi na hata wazazi wa pande zote mbili wanafahamu uhusiano wao.

Kuna kitu kimoja(akicheka kidogo), sasa hivi haya mambo ya mtandao yanapotosha sana jamii kwa upande mwingine na pia watu wamejua maisha ya kila mtu kuyaweka kwenye mtandao, labda niseme sijui watu wanataka waone vile mimi naishi jinsi wanavyotaka wao, kitu ambacho hakiwezekani, lakini suala zima la kuachana na Ray, hapana tuko wote”, alisema Chuchu

Ameongeza kuwa hata sababu zinazotajwa kama ushahidi wa kuachana kwao, kama vile kutopostiana tena picha na kutotoka tena out wakiwa pamoja kama vile walivyokuwa wakifanya hapo awali, amesema kuwa ni ubize wa kazi ndio unachangia kutokea kwa ishu hiyo.

Naweza nikarudi tena palepale, ile ilikuwa ni Desemba, ilikuwa ni holiday sio kipindi cha kazi, kwaiyo sasa hivi tunafikiria tufanye nini, kwaiyo hata sasa hivi kutoka kidogo tumepunguza, sasa hivi kutoka ni mara moja moja sana, Ray ana-handle kampuni mbili, kuna hii ya RJ ambayo ni kampuni mama na Chura”.

Aidha amesema kwamba hana kabisa kinyongo na Johari aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Ray enzi hizo.  Pia amefafanua suala zima la kuachana na mume wake ‘Frank Mtawa’ na kusema kwamba baba watoto wake huyo ambaye amehamishia makazi yake  nchini Australia tayari amekwishavuta jiko.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s