A.Y ATOA DUKUDUKU LAKE JUU YA BARABARA ZA MTAANI

Ambwene YesayaStaa nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya ‘A.Y’  ametoa dukuduku lake juu ya barabara za mtaani ambazo hazipo katika kiwango kizuri wakati akizungumza katika sejimenti ya Dukuduku ya Capital Fm.

Msanii huyo amesema sio  lazima mpaka serikali ifanyie ukarabati barabara hizo na badala yake wananchi au wakazi wa eneo husika wanaweza wakachangishana fedha kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya barabara zao.

Serikali ni wananchi, kwa sababu wananchi ndio wanaoamua kila kitu, wananchi kwa mfano wa mtaa flani labda unaitwa X, mtaa wanachanga katika mwaka mmoja, jamani eeh mwakani tunataka kubadilisha barabara zetu katika mtaa wetu, mmiliki wa kila nyumba kutokana hata na kodi au wao wanavyoishi na kufanya kazi, wanatoa laki tano tano, tunaweka lami ya kiwango cha kati, sio lami kubwa kama hizo zingine”, alisema A.Y .

Aliongeza : ”mnatengeneza barabara vizuri, mnatengeneza mitaro vizuri na mwisho wa siku barabara itapendeza hata kiwango cha kodi pia kitaongezeka lakini mwisho wa siku unakuta mitaa inanyumba za gharama kubwa, lakini mwisho wa siku nje ya nyumba barabara ni mbaya, zina makorongo, zinaweka maji wakati wa mvua ni kitu ambacho kinanifanya mwenyewe niwe na dukuduku langu”.

Pia  A.Y ametolea mfano wa nchi kama ya Kenya ambao  wanautaratibu kama huo aliouelezea na ndio maana barabara nyingi za ndani nchini humo zipo katika kiwango kizuri tofauti na hapa Bongo.

Je, kwa upande wako wewe msomaji, hili dukuduku la Ambwene Yesaya wewe unalitazamaje??? linawezekana??? au haliwezekani???.  Mwaga maoni yako hapo chini

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s