LIL WAYNE AIDAI CASH MONEY FIDIA YA DOLA MILIONI 51 ZA KIMAREKANI

New Orleans rapper Lil Wayne sits with Birdman during the New Orleans Hornets NBA basketball game against the Miami Heat in New OrleansWahenga wanakwambia,Heri ufe umesimama ukidai haki yako kuliko kufa umelala kwa njaa.  Rapa Lil Wayne amemfungulia rasmi mashtaka baba yake wa hiyari ‘Birdman’ akitaka kuachiwa huru kutoka katika lebo ya Cash Money.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Wayne anadai Birdman alikuika masharti ya mpango wao kwa kuzuia mamilioni ya dola  anayoidai Cash Money kutokana na kuchelewa kuiachia albamu yake mpya, Tha Carter V.

Tangu Cash Money ikatae kumlipa , Wayne anasema ana haki ya kuvunja mkataba vilevile ameishtaki lebo hiyo fidia ya dola milioni 51 za kimarekani.

Wayne amemtaka hakimu kumpa umiliki wa hati miliki ya wa wasanii wote waliopo Young Money wakiwemo Drake, Nicki Minaj, Tyga, Gudda Gudda na wengine zaidi.  Amepanga kuwachukua wasanii wake kutoka Cash Money.

Hata hivyo, Kama  Birdman atalipa kiasi hicho cha fedha anazodaiwa, Kambi ya Wayne itaruhusu Cash Money kuachia albamu ya Tha Carter V. 

Wayne alitakiwa apate dola milioni 8 kama malipo ya awali wakati alipoanza kurekodi Decemba 2013 na dola milioni 2 baada ya kumaliza albamu mwaka mmoja baadaye, lakini hadi sasa hajapokea hata senti tano.

 

 

Advertisements

2 thoughts on “LIL WAYNE AIDAI CASH MONEY FIDIA YA DOLA MILIONI 51 ZA KIMAREKANI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s