LUDA ASHINDA KESI, APEWA KIBALI NA MAHAKAMA CHA KUISHI NA BINTI YAKE

LudaHatimaye Rapa Ludacris amepewa kibali na mahakama cha kuweza kuishi na mtoto wake wa kike ‘Cai’ baada ya kusumbuana kwa muda mrefu kortini na mzazi mwenzake aliyekuwa akipinga vikali suala hilo.

Ishu hiyo inakuja kufuatia mama wa mtoto, Tamika Fuller  kutoa ushahidi mapema leo kwamba aliahidiwa dau la dola za kimarekani 10,000  na nyumba kutoka kwa mwanamuziki huyo ili aichoropoe mimba.

Wakili wa Luda, Tanya Mitchell Graham, alitoa taarifa rasmi kwa Sandra Rose, kuthibitisha habari hizo.  Taarifa hiyo ilisomeka, Baada ya mapitio ya ushahidi wote, ushahidi wa mashahidi, ripoti ya mlezi, na madai yaliyotolewa katika kesi nzima, nimeridhishwa kwamba hakimu ameona nafaa na kimsingi kuwa mzazi sahihi mwenye mamlaka ya kumtunza mtoto wetu mzuri”.

Kwa ushindi huo, Cai mwenye umri wa mwaka mmoja ataungana na familia ya Luda na mke wake Eudoxie katika mjengo wao na kuweza kupatiwa haki zake za msingi anazostahili kama mtoto, huku Fuller akibakiwa na nafasi ya kumtembelea.

Hata hivyo uamuzi uliotolewa na mahakama umeonekana kuwashangaza watu wengi waliokuwa wakitarajia Tamika angelipewa nafasi ya kumlea mtoto wake huyo aliyemkuza kwa takribani miezi kumi na tatu na kudai yote ni kutokana na mwanamke huyo kuzidiwa mkwanja mtu mzima Luda.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s