EX WA NICKI MINAJ AJISAFISHA KIAINA, ‘SIJAWAHI KUMUANDIKIA MINAJ MASHAIRI’.

Nicki Minaj Safaree Samuels

Safaree Samuels na Nicki Minaj enzi za mapenzi yao

Aliyekuwa mpenzi wa Rapa wa kike, Nicki Minaj, Safaree Samuels amegeuka kigeugeu baada ya kuikana kauli aliyoitoa wakati alipofanyiwa mahojiano katika kipindi cha redio cha The Breakfast Club,  pale alipodai enzi za mapenzi yao alikuwa akimsaidia diva huyo wa Young Money kumtungia mashairi flani amazing katika nyimbo zake.

Usiseme sina kipaji, kwa sababu kila mara linapokuja suala la kuandika mashairi na kufanya muziki, nilikuwa mimi, yeye(akimaanisha  Minaj) na Beat, alikuwa hawezi kuandika mashairi mwenyewe”, alisema Samuels katika interview aliyofanyiwa na mtangazaji Angie Martinez wiki mbili zilizopita.

Aidha Samuels amemuomba msamaha Minaj juu ya yale mabaya aliyoyasema kwenye interview alizofanyiwa hapo awali na kumfagilia kuwa ni mtu mzuri na mwenye kipaji cha hali ya juu.

Kama kuna kitu chochote kilimkwanza Nicki  katika mahojiano yangu, naomba radhi na nataka watu waelewe kwamba yeye alikuwa mtu mzuri ”, alindika Samuels katika ukurasa wake wa Twitter na kuongeza,”Sijawahi kusema niliwahi kumuandikia mashairi, yeye ni mtu mzuri ndani na nje na mtu mwenye kipaji ninayemfahamu”. 

Pia amewaponda wale mashabiki waliokuwa wakimfuatilia kwa kuwaita wajinga na kuwataka wamuache aendelee na maisha yake.  Unaweza ukatazama  Tweets alizoandika sharobaro Safaree  kwenye ukurasa wake wa Twitter aki-apologize kwa mtoto mzuri Nicki minaj hapo down.

Tweets Tweets1 Tweets2

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s