WEMA SEPETU AOMBWA RADHI NA GAZETI LA MTANZANIA

Wema SepetuGazeti la Mtanzania limemuomba radhi mwanadafada Wema Sepetu baada ya kuchapisha stori kuwa amempeleka mahakamani aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz kwa kushindwa kulipa deni la shilingi milioni 10 alizomkopea VICOBA.

Akitiririka kwenye 255 ya Clouds Fm, Meneja wa Sepetu, Martin Kadinda amesema tayari mwanasheria wa kampuni yao ya Endless Fame amekwishafungua kesi ya kuchafuliwa kwa jina la Wema, licha ya kupigiwa simu na waandishi wa gazeti hilo wakimuomba radhi na kuwataka wamuombe radhi Wema mwenyewe kwa ukubwa ule ule wa stori.

Kwa sababu tayari tuna mwanasheria wa kampuni ambaye amekwisha file kesi kwa kuweza kuchafua jina la Wema pamoja na mwenzi wake aliyekuwa nae kwa kipindi hicho, kwa sababu hiyo ni conflict ya biashara, lazima Diamond kwa upande wake amechafuliwa jina na pia kwa upande wetu tumechafuliwa jina”, alisema Martin Kadinda

Aliongeza :Ni watu waliamua kutengeneza ile link kwa ajili ya hiyo Saccos yao, kwa hiyo wale walikopi stori iliyoandikwa na mtu mwingine na walinipigia simu wakaniuliza, nikawambia hiyo taarifa haina ukweli wowote lakini ili kuweza kupata uhakika naomba wema ataongea na nyinyi, lakini kabla sijafanya mawasiliano, nao wakawa wameshatoka na stori. Kwaiyo nikasema either wamuombe radhi Wema kwa ukubwa ule ule wa stori waliokuwa wameuandika mara ya kwanza na pia watoe tamko wao kwamba  stori ni ya uongo na haina ukweli wowote”.

Baada ya kuona jitihada za kuomba msamaha kimya kimya zimegonga mwamba, gazeti la mwananchi ilibidi wachapishe habari iliyokuwa ikimuomba radhi Wema Sepetu na familia yake kwa kumchafua kimakosa kutokana na kupotoshwa na chanzo kilichowapatia habari zake.

Katika gazeti letu la Mtanzania tolea namba 7709 la alhamisi Januari 22 mwaka huu, tuliandika kimakosa stori yenye kichwa cha habari  ‘WEMA SEPETU AMPELEKA DIAMOND POLISI” baada ya kufanya uchunguzi tumejiridhisha habari hiyo haikuwa ya ukweli kwani chanzo kilichotupatia kilitupotosha, hivyo kuleta usumbufu wa msanii Wema Sepetu pamoja na jamii.  Kutokana na hali hiyo tumependa kumuomba radhi Wema Sepetu na familia yake, Siku zote sisi Mtanzania tumekuwa makini katika kuandika habari za uweledi na haki kwa jamii,” liliandika gazeti la Mtanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s