SARE YA MOJA MOJA YAZIPELEKA CONGO DRC NA TUNISIA ROBO FAINALI, CAPE VERDE, ZAMBIA ZAFUNGASHA VIRAGO

Congo Vs Tunia

Mshambuliaji wa Tunisia, Ahmed Akaichi mwenye jezi nyeupe akiruka juu kuwania mpira na mchezaji wa Congo katika mchezo uliomalizika kwa sare ya moja moja

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yenye pointi 3 imesonga mbele baada ya kupata sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Tunisia na kuizidi Cape Verde kwa magoli ambayo ilitoka suluhu dhidi ya Zambia huku vinara tunisia wakiongoza kundi wakiwa na jumla ya pointi tano.

Congo DRC  na  Tunusia  zimesonga  mbele baada ya  kutoka  sare, huku Zambia na  Cape Verde  zikifungasha virago  katika  kundi B.

Kocha wa timu ya Taifa ya Congo, Florent Ibenge , amekiri kuwa wametinga hatua ya robo fainali kwa mbinde licha ya vijana wake kupigana kufa na kupona kutokana na upinzani mkali katika mechi za kundi ”B” kwenye michuano ya AFCON inayoendelea kutimua vumbi nchini Guinea Equator.

Kocha Ibenge anasema anajiandaa kuwakabili majirani zao Congo Brazaville inayoongozwa na kocha Claude Le Roy ambaye ametinga hatua hiyo mara nane katika michuano ya Afcon akiwa na timu mbalimbali.

Tunisia mabingwa wa Afcon mwaka 2004, watapambana na wenyeji wa michuano hiyo Guinea Equator katika robo fainali ya kwanza.

Wakati huo huo, golikipa nambari moja wa Zambia, Kennedy Mweene amekanusha uvumi wa kutundika daruga mara baada ya timu yake kutolewa mapema kwa mara ya pili mfululizo katika michuano ya Afcon.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s