PROF.LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI DAR AKIDAIWA KUSHAWISHI WAFUASI WA CUF KUANDAMANA

Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF, Prof Ibrahim haruna Lipumba akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo alipofikishwa kusjibu shitaka la kuhamasisha wanacham awa chama chake kufanya jinai.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF, Prof Ibrahim haruna Lipumba akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo alipofikishwa kusjibu shitaka la kuhamasisha wanacham awa chama chake kufanya jinai.

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Kisutu na kusomewa shitaka moja la kuwashawishi wafuasi wa chama hicho kufanya maandamano kati ya Januari 22 na 27 mwaka huu.

Wakili wa serikali Joseph Maugo amesema kosa hilo la kushawishi na kutenda kosa lipo katika ibara ya 360 kifungu cha 35 cha kanuni ya adhabu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kusomewa shtaka, Profesa lipumba alikana shtaka hilo ambalo hakimu mkazi aliweka wazi dhamana kwa mshtakiwa ambapo wadhamini wawili walijitokeza na kumdhamini kila mmoja kiasi cha shilingi milioni 2, huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa Februari 26 mwaka huu.

Ukweli ni kwamba nchi yetu haina haki, na kesi hizi ni kesi za kubambikiziwa, lakini mambo hayo tutayazungumza mahakamani”, alisema Profesa Lipumba nje ya viunga vya mahakama ya Kisutu.

Awali katika kituo cha polisi cha kati, wafuasi 32 waliokamatwa jana waliruhusiwa kwa dhamana saa 5 usiku, ambapo walitakiwa kuripoti kituoni hapo huku ulinzi wa polisi ukiimarishwa katika eneo hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s