MAYWEATHER, PACQUIAO WAKUTANA USO KWA USO NA KUSALIMIANA

Pacquiao na Mayweather

Mayweather akisalimiana na Manny Pacquiao

Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wameudhihirishia ulimwengu kuwa uhasama uliopo kati yao ni wa ulingoni na sio sehemu nyingine, hiyo ni baada ya kukutana uso kwa uso na kusalimiana kama vile sio mahasimu wakubwa.

Mabondia hao wanaoshikilia mataji makubwa ya ndondi Duniani,  walikutana katika uwanja wa American Airlines usiku wa kuamkia leo(Jan27) wakati wa mchezo kati ya timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat na  Milwaukee ambao ulimalizika kwa Bucks kushinda jumla ya vikapu 109 – 102 dhidi ya Heat.

Mbali na mchezo huo, mashabiki na wapenzi wa masumbwi Duniani kote wamekuwa wakisubira kwa hamu mpambano wa wawili hao ambao wamekuwa wakitambiana kwa kipindi kirefu unaotajwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.  Watazame hapo chini wakisalimiana

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s