LIL WAYNE KUWACHUKUA DRAKE NA NICKI MINAJ KUTOKA CASH MONEY

Drake Minaj Lil Wayne

Rapa Lil Wayne ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka kuihama lebo ya Cash money inayomilikiwa na Birdman na kuongeza kwamba ataondoka na marapa wenzake ambao ni Drake pamoja na Nicki  Minaj.

Wayne ambaye ni C.E.O wa Young Money, amepanga kumshtaki Birdman kwa kitendo cha kutotaka kumuachia katika lebo yake sambamba na madai ya dola za kimarekani milioni 8 kama sehemu ya malipo ya awali kwa ajili ya albamu yake mpya  ya The Carter V ambayo bado haijatoka.

Aidha Rapa huyo amedai atahakikisha wasanii wote wa Young Money wanakuwa chini yake kwa sababu mikataba yao iko chini ya lebo yake.

Hata katika remix ya wimbo wake wa Coco unaopatika katika mixtape yake mpya ”Sorry 4 the wait 2”, Wayne anasema, ”I Ain’t trippin’, I got Barbie, I got Drake too”.  Akiamini  kwamba Drake na Nicki hawatoweza kumsaliti.

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s