BUNGE LAAHIRISHWA KABLA YA MUDA KUTOKANA NA TUKIO LA KUPIGWA WAFUASI WA CUF

James Mbatia

Mwenyekitii wa chama cha NCCR-Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia akitoa hoja bungeni mjini Dodoma

Bunge la jamhuri la muungano wa Tanzania leo lilihairisha kikao chake kufuatia wabunge wa upinzani kutaka kujadiliwa kwa hoja ya kupigwa na polisi, wafuasi na viongozi wa chama cha wananchi ‘CUF’ huku spika akitaka mjadala huo kufanyika kesho baada ya serikali kutoa taarifa.

Hali hiyo ilitokana na kuwasilishwa kwa hoja na mbunge wa kuchaguliwa ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia akitaka shughuli zote zilizopangwa zihairishwe ili kutoa nafasi kwa bunge kujadili jambo la kupigwa kwa wananchi na wafuasi wa chama cha CUF.

Hata hivyo pamoja na wabunge wa upinzani kuiunga mkono hoja hiyo, spika wa bunge Anna Makinda akatoa ufafanuzi kuhusiana na kanuni iliyotumiwa na kusisitiza kuwa kulikuwa hakuna haja hoja hiyo kuungwa mkono.

Kutokana na kushindwa kufikia muhafaka na wabunge hao, Spika Makinda ilimbidi kulihairisha Bunge mpaka kesho.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s