WAKAZI : HOMA YA DENGUE ILINIFANYA NIITUNGIE WIMBO

Wakazi BBA

Rapa Wakazi akitumbuiza katika jumba la Big Brother kwenye shindano la BBA The Chase mwaka juzi

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo mwenye makazi yake Ukonga jijini Dar es salaam, Webiro Wakazi amesema kipindi anaandika ngoma yake mpya ‘Dengue Fever’ alikuwa akiumwa ugonjwa huo unaosambazwa na mbu aina ya Aedes Aegypti ambao ulipata kuwa habari ya mjini.

Wakazi amepasua kwamba, kitu kikubwa alichozungumzia ndani ya wimbo huo ni kuonyesha ni jinsi gani alivyoshindikana na kupitiliza.  Moja ya mistari katika ngoma hiyo  unasema, ”Niite mbu wa mchana A.K.A Dengue Fever’‘.

Niliumwa Dengue Fever, sikujitangaza lakini niliumwa Dengue Fever, wakati naumwa ndio nikawa natunga haya mashairi”, Wakazi alifunguka kwenye kipindi cha X-Ray ya EFM

Pia msanii huyo amezungumzia experience aliyopata wakati alipopata shavu la kutumbuiza katika shindano la Big Brother Africa The Chase mwaka juzi.

Wanasemaga nabii hakubaliki kwao, kwaiyo mimi nilikuwa nafanyia muziki toka niko nje, nazituma nyimbo za mixtape, lakini nikarudi nikatoa audio na video kali lakini nikaona bado upokelewaji wangu upo so so hivi wa uvuguvugu”, alisema Wakazi

hasa watu wa nje, kwa sababu nilikuwa najinadi kwenye mitandao ya kijamii,watu wa nje wao kunipa nafasi kubwa kama ile kwenda Big Brother, ikanionyesha nachokifanya sio kwamba ni kibaya, sema labda tuu home watu hawajaelewa, lakini si kwamba mimi hapa sieleweki ,  kwa sababu wao wameamua kunielewa kwaiyo ilikuwa na nafasi nzuri sana kwangu”.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s