KIMENUKA CASH MONEY : LIL WAYNE ATISHIA KUMBURUZA BIRDMAN MAHAKAMANI

Lil Wayne X BirdmanHali imeonekana kuwa si shwari katika lebo ya Cash Money, baina ya  Rapa Lil Wayne na baba yake wa hiyari ‘Brayan Adams’ A.K.A Birdman hadi kufikia hatua ya kutaka kuburuzana mahakamani.

Upepo mbaya ulianza kuvuma baada ya Lil Wayne kuanza kulalamika juu ya albamu yake mpya ”The Carter 5′‘  kucheleweshwa kutoka, ambapo ilitakiwa iingie rasmi sokoni mwishoni mwa mwaka jana.

Kama hiyo haitoshi, Mapema wiki hii, Weezy aliamua kuwaomba msamaha mashabiki kutokana na kuchelewa kutoka kwa albamu hiyo  kupitia mixtape yake mpya ”Sorry 4 The Wait 2”  ambapo ndani yake amem-diss mtu mzima Birdman kwenye ngoma inayoitwa Coco na kujigamba kwamba yeye ni jeshi la mtu mmoja.

All I got is Young Money, no more Cash nigga,” “Who kept this s**t together? N***a, me, that’s who! Who was there when n***as left? N***a, me that’s who!” Cash Money is an army, I’m a one man army!“.

Hata hivyo Birdman ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutotaka kuiachia albamu ya rapa huyo mpaka siku atakayoamua yeye kuitoa na kudai kuwa Weezy bado yupo chini ya mkataba na lebo yake.

Hali iliyompelekea Weezy kuanza kutafuta msaada wa kisheria wa kutaka kuiomba mahakama iweze kumsaidia kutoka katika lebo ya Cash Money na kutokuwa chini ya utawala wa Birdman ambaye ameendelea kuishikilia albamu yake.

Akiamini kuwa bado anamdai Birdman kiasi cha dola milioni 8 kama sehemu ya malipo ya awali kwa ajili ya albamu hiyo huku kukiwepo na tetesi za Rapa huyo kutaka kuhamia katika lebo ya No Limit inayomilikiwa na Master P.

Endelea kutembelea Blogu yako ya kijanja ya Larrybway91  kwa muendelezo wa habari hii na nyinginezo kibao zinazowahusu mastaa mbalimbali wa hapa bongo na nje.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s