BREAKING NEWZ : WAZIRI MUHONGO ATANGAZA KUJIUZULU WADHIFA WAKE

Profesa Sospeter MuhongoWaziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake hii leo kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Waziri Muhongo ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam huku akisema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira mazuri kwa Tanzania kuwa kipato cha kati katika uchumi kupitia ugunduzi wa gesi asilia ya huko mkoani Mtwara.

Shinikizo la kijiuzulu kwa waziri huyo limo katika maadhimio manane ya Bunge yaliyofikia katika kikao cha 16 na 17 kilichomalizika mwishoni mwa mwaka jana mjini Dodoma.

Miongoni mwa maadhimio hayo, Bunge lilizitaka mamlaka husika kuwawajibisha watendaji serikalini waliohusika katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 300 zilichotwa na watu wachache katika akaunti hiyo.

Tayari mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema ameshajiuzulu huku waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akifukuzwa kazi kufuatia sakata hilo la Escrow.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s