JUSTIN BIEBER AMFUNIKA KIM KARDASHIAN KWA KUZUNGUMZIWA ZAIDI MITANDAONI

Mwanamitindo na staa wa Keeping up With The Kardashians, Kim Kardashian amefunikwa na mwanamuziki Justin Bieber katika suala zima la kuzungumziwa zaidi mtandaoni.

Kim Kardashian - Paper Magazine

#BreakTheInternet : Picha ya Kim Kardashian ambayo ilitumika kukava jarida la Paper mwezi Novemba mwaka jana

Imeonekana watu wengi walivutiwa zaidi na picha za Justin Bieber akiwa ametinga boksa ya Calvin Klein katika kampeni ya kutangaza mavazi  ya kampuni hiyo  kuliko picha za utupu za Kim ambazo zilitumika kukava kurasa za mbele za jarida la paper.

Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, Kim Kardashian ali-break the internet baada ya picha hizo kupata kiki ya kuzungumziwa zaidi, kabla ya Bieber kufanya mageuzi makubwa mapema mwezi Januari mwaka huu kwa picha zake akiwa ametupia boksa za Calvin Klein.

Kwa mujibu wa tovuti ya Women’s Wear Daily, imeeleza kwamba Kampeni ya Bieber ilipata kuzungumziwa sana katika mitandao ya kijamii kuliko ya Kim K.

Justin Bieber

#Mycalvin : Picha ya Justin akiwa ametinga boksa ya Calvin Klein katika kampeni ya kuzitangaza nguo za ndani za kampuni hiyo

Tovuti hiyo imesema, ”Katika masaa 48 ya kwanza baada ya uzinduzi, hashtag ya #Mycalvins ilitajwa zaidi ya mara milioni 1.6 katika mtandao wa  Twitter ikiwa ni mara tano zaidi ya picha za Kim akiwa amesaula zilizotumika kukava jarida la Paper kupitia hashtag ya #Breaktheinternet.

Pia tovuti hiyo imeongeza kuwa, tangu kampeni hiyo kuzinduliwa, Channel za kwenye mitandao za kampuni ya Calvin Kleins kama vile Youtube zimeongeza zaidi ya wafuasi milioni 3.6 kila moja.

Je, unakubaliana na kampeni ya Justin Bieber kuzungumziwa zaidi ya mwanadafada Kim licha kusaula kila kitu??? Mwaga maoni yako hapo chini

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s