DJ FUNKMASTER FLEX AMPA MAKAVU JAY Z BILA KUPEPESA

Jay Z Funkmaster FlexDj maarufu wa kituo cha Hot 97, Funkmaster Flex, ameamua kutumia muda wa kipindi chake kumponda Rapa Jay z kwa madai ya kumuibia wazo lake la application ya kwenye simu.

Alhamisi iliyopita Flex alitumia takribani lisaa lizima ya kipindi chake kumponda Jay Z na tovuti yake ya Life & Times na kusema kwamba hiyo yote ilianza miaka ya nyuma kidogo wakati akiwa na application yake ya Dj Funkmaster Flex.

Dj huyo mkongwe wa New York aliendelea kupasua na kudai kuwa alipata barua pepe toka kwa waandishi wa tovuti ya Jay Z wakitaka kufanya nae mahojiano kuhusiana na kujihusisha kwake na masuala ya kutengeneza applications na mambo mengine.

Alisema zilikuwa ni mbinu za kutaka kunasa taarifa hizo ambazo ziliwekwa kwenye application mpya ya Jay Z ambayo ilitumika kuachia albamu yake ya Magna Carter Holly Grail kupitia dili yake na Samsung.

Lakini cha kushangaza msaidizi wa Flex alipokea tena email kutoka kwa wafanyakazi wa Life & Times wakitaka kufanya mahojiano nae juu ya  kujihusisha kwake na kundi la Dipsett kuhusiana na muungano wao utakaofanywa rasmi mwezi ujao ambao ni mahasimu wakubwa wa Jay Z.

Kitendo kilichozidi kumtia jazba Dj huyo na kudai hata kipindi alipokuwa akifanya kazi katika klabu za Jay Z ”40/40” alikuwa akikatazwa kupiga ngoma zao.

Mimi sio mpumbavu, usicheze na mimi, nitakupoteza,  nakuachia tuu uishi New York”, alisema FLex ukiwa ni ujumbe kwenda kwa Rapa  Jay Z ambaye amenukuliwa siku za hivi karibuni kutaka kununua kituo cha Radio cha Hot 97 ambacho anafanyia kazi Funkmaster Flex ikiwa ni kutaka kumkomoa.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s