CAPITAL ONE CUP : LIVERPOOL, CHELSEA ZATOKA SARE YA MOJA MOJA

Amra Can baada ya kumkwatua Hazard

Can akimfanyia madhambi Hazard kabla ya Chelsea kupewa penalti iliyopigwa na mbelgiji huyo 

Michuano ya kuwania kombe la Capital One inaelekea ukingoni baada ya jana miamba ya Uingereza, Liverpool  na  Chelsea kushuka dimbani katika hatua ya nusu fainali.

Chelsea wakiwa ugenini ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Liverpool kwa njia ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Eden Hazard kufuatia madhambi aliyofanyiwa na Emre Can ndani ya boksi.

Hata hivyo haikuwa bahati kwa Chelsea baada ya mshambuliaji wa majogoo hao wa jiji la London, Raheem Sterling  kusawazisha mnamo dakika ya 59 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya moja moja.

Timu hizo zinatarajia kurudiana Jumanne ijayo(Jan 27) nyumbani kwa Chelsea ‘Stamford bridge’ wakati Tottenham ikijiandaa kuivaa Sheffield hii leo katika nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo.

Eden Hazard

Hazard akishangilia baada ya kuipatia Chelsea bao la kuongoza kwa njia ya mkwaju wa penalti  dhidi ya Liverpool

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao

Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza Hazard kwa kufunga bao la kuongoza ugenini dhidi ya majogoo wa jiji la London

Raheem Sterling

Mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling, akishangilia mara baada ya kuisawazishia timu yake mnamo dakika ya 59 katika dimba la Anfield

Wachezaji wa liverpool

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia goli la kusawazishwa lililofungwa na Sterling

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s