MUIGIZAJI NYOTA WA NOLLYWOOD ‘MUNA OBIEKWE’ AFARIKI DUNIA KWA MARADHI YA FIGO

Muna Obiekwe

Muigizaji Muna Obiekwe enzi za uhai wake

Muigizaji nguli  wa kiwanda cha filamu Nollywood, Muna Obiekwe, amefariki Dunia Jumapili(Jan.18) majira ya saa kumi jioni mjini Lagos nchini Nigeria.

Obiekwe mwenye umri wa miaka 36, alidondoka ghafla wakati akiwa nyumbani kwake na hivyo kuwalazimu ndugu zake kumkimbiza hospitali kabla ya kufikwa na umauti

Kwa mujibu wa familia ya marehemu imesema kuwa, Obiekwe alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu ingawa hakuwahi kuomba msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu au kuwaambia marafiki zake kuhusiana na ugonjwa wake.

Wadau, Mashabiki na Mastaa mbalimbali wa Afrika wameonyesha kuguswa na msiba huo na kutoa salamu zao za pole kwa familia ya marehemu kupitia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Instagram na Facebook akiwemo Genevieve Nnaji, Rita Dominic, Stella Damscus, Rugged Man, Uche Jombo, Van Vicker, Uduak Isong na Dayoa Musa

Marehemu Obiekwe atakumbukwa kwa umahari wake wa kuuvaa uhusika pindi anapokuwa mbele ya kamera akiwa amekwisha igiza  filamu lukuki kama vile Pregnant Hawker, Secret Shadows, Scarlet Woman, Great Betrayal, Return of Destiny Call na nyingine kibao.

Advertisements

One thought on “MUIGIZAJI NYOTA WA NOLLYWOOD ‘MUNA OBIEKWE’ AFARIKI DUNIA KWA MARADHI YA FIGO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s