WATU 10 WAUWAWA NA MAKANISA KUCHOMWA MOTO KATIKA GHASIA NCHINI NIGER

NigerWatu 10 wameuwawa na makanisa kuchomwa moto katika ghasia zilizozuka Niger wakati wa maandamano ya kupinga chapisho la la gazeti la Charlie Hebdo.

Rais wa Niger ‘Mahamadou Issoufou’ amelaani kitendo cha waumini wa kiislamu kufanya maandamano ya fujo yaliyosabbaisha vifo na kujeruhi watu kadhaa.

Maandamano hayo yalikuwa na nia ya kupinga hatua ya gazeti la Charlie Hebdo kuchapisha tena kikatuni kwenye ukurasa wake wa mbele kilichomaanishwa kuwa ni Mtume Muhammad.

Watu 5 wameuwawa, makanisa kadhaa kuharibika katika maandamano yaliyofanywa jana sehemu mbalimbali za Niger.

Hayo yamefuatia machafuko yaliyotokea siku moja iliyopita katika mji wa Zinder ambao ni wa pili kwa ukumbwa nchini Niger ambapo watu wengine 5 waliripotiwa kuuwawa huko Zinder.

Niger Church

Kanisa lililopo nchini Niger baada ya kuchomwa moto na waandamanaji wa kiislamu

Niger Ghasia

Gari likiteketea kwa moto kufuatia kuchomwa na waandamanaji

Niger Polisi

Gari la polisi likitetekea kwa moto nchini Niger kufuatia ghasia za waumini wa dini ya kiislamu kupinga kitendo cha jarida la Charlie Hebdo la ufaransa

.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s