RAPA A$AP YAMS AFARIKI DUNIA

Tasnia ya muziki wa Hip-Hop Duniani imepata pigo la kuondokewa na rapa wa kundi la A$AP Mob, A$AP YAMS, ambaye amefariki Dunia  leo(Jan.18) huko Marekani.

A$ap YamsMmoja wa wanafamilia wa kundi hilo, A$ap Bari alivujisha taarifa kuhusiana na kifo cha Yams ambaye alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa kundi hilo, lakini hadi sasa, bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.

Kwa mujibu wa tovuti ya MissInfo, Yams ambaye jina lake halisi ni Steven Rodriguez, alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya aina ya Codeine na Xanax.

Tovuti hiyo imesema kwamba Rapa huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwahi kupatiwa matibabu kwenye kituo tiba ‘Rehab’ katika kipindi kifupi cha majira ya joto mwaka jana katika jitihada za kukabiliana na madawa ya kulevya.

Hata ujumbe wa mwisho aliouandika marehemu Yams katika ukurasa wake rasmi wa Twitter hiyo jana ulikuwa ukihusu madawa ya kulevya.  ”Bodeine Brazy”, aliandika Yams

Wasanii mbalimbali wametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu kupitia mtandao wa Twitter wakiwemo vinara wa kundi hilo, A$ap Rocky  na A$ap Ferg ambao wameonyesha kusikitishwa zaidi na taarifa hizo.

A$AP Yams(Wa Kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na wanafamilia wa kundi la A$AP Mob

A$AP Yams(Wa Kwanza kushoto) enzi za uhai wake katika picha ya pamoja na wanafamilia wa kundi la A$AP Mob

A$ap Yams

A$AP FERG Tweet

Twitter

Tweets

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s