AFCON 2015 : GUINEA, CONGO ZATOKA SARE, GABON YAICHAPA BAO 2 – 0 BURKINA FASO

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ‘AFCON’ 2015 imeanza kutimia vumbi baaada ya wenyeji Equatorial Guinea kushuka dimbani na kukipiga na timu ya taifa ya Congo wikiendi iliyopita katika mchezo wa ufunguzi nchini humo.

Mshambuliaji wa Guinea, Emilio Nsue aliyevaa jezi nyekundu akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza

Mshambuliaji wa Guinea, Emilio Nsue aliyevaa jezi nyekundu akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza

Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya bao moja moja, ambapo Guinea walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za wapinzania wao kupitia mshambuliaji wake ‘Emilo Nsue’ kabla ya kusawazishwa na Thievy Bifouma wa Congo.

Mtanange mwingine uliopigwa siku hiyo  ni ule uliowakutanisha Burkina Faso ambao walikubali kipigo cha jumla ya mabao mawili kwa mtungi toka kwa Gabon. 

Mabao ya Gabon yaliwekwa kimyani na Winga wa Borussia Dortmund ‘Pierre-Emerick Aubameyang’ na Malick Evouna.

Halaiki

Kikundi cha ngoma za asili wakifungua rasmi michuano ya AFCON 2015 katika uwanja wa Bata uliopo nchini Equatorial Guinea

Mashabiki wa Guinea

Mashabiki wa Guinea wakiishangilia timu yao katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s