SIMBA MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2015

Simba Sc Mapinduzi CupWekundu wa msimbazi ‘Simba Sc’ wameibuka mabingwa wa kombe la Mapinduzi baada ya kuilaza Mtibwa Sukari ya Morogoro kwa mikwaju ya penalti katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Amani visiwani Zanzibar usiku wa kuamkia leo(Jan.13).

Mpaka dakika 90 zinamalizika sio Simba wala Mtibwa ambaye alifanikiwa kutikisa nyavu za mwenzake. Kipa wa Simba, Ivo Mapunda ameweza kuibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kufuta mikwaju miwili ambayo ilipigwa na  Rajab Jeba pamoja na Vicent Barnabas wote wa Mtibwa baada ya kuchukua nafasi ya golikipa Peter Manyika mnamo dakika ya 90.

Wakati kwa upande wa Simba wakipoteza mkwaju mmoja uliopigwa na Shabani Kisiga na kufanya matokeo kumalizika kwa wekundu hao wa msimbazi kuibuka bingwa kwa jumla ya mikwaju minne ya penalti dhidi ya mitatu.

Kwa matokea hayo yanaifanya timu ya Simba kuendelea kushikilia rekodi yake ya kuifunga Mtibwa mara mbili katika michuano hiyo ya Mapinduzi.

Simba Sc walikabidhiwa kombe lao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein  na zawadi ya shilingi milioni 10 kwa kutwaa ubingwa, wakati Mtibwa  ikiambulia shilingi milioni 5 za kibongo kama zawadi ya mshindi wa pili.    

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s