CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA FIFA BALLON D’OR KWA MARA YA TATU

Cristiano RonaldoMshambuliaji  wa kimataifa wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia maarufu kama FIFA Ballon D’or kwa mara ya tatu  katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kongresshaus mjini Zurich,  nchini Uswisi.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 29, ameifungia timu yake ya Madrid inayoshiriki ligi kuu ya Hispania ‘La Liga’ jumla ya mabao 31 katika michezo 30 ambayo alicheza katika msimu huu na kuwagalagaza wapinzani wake ambao ni Straika wa barca, Lionel Messi na kipa ‘Manuel Neuer’ anayeidaikia klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. 

Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuibuka mshindi wa Tuzo hiyo kwa kupata Kura asilimia 37.66, Messi 15.76 na  Neuer kura 15.72.

Pindi unaposubiria kusikia jina likitajwa, ni wakati mgumu”, alisema Ronaldo na kuongeza, ”Najua ni kiasi gani bidii ya kazi na jitihada ambazo zimenifanya nishinde tuzo hii, na ndio maana bado napatwa na hisia, haijalishi ni mara ngapi nimekuja hapa kuipokea, natumaini nitafanya hivyo kwa miaka mingi ijayo”.

Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ureno kuchukua Tuzo hizo mara nyingi ikiwa ni mara yake ya tatu baada ya kufanya hivyo mwaka 2008  na 2013

Pia Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa  ligi kuu barani Ulaya baada ya kufunga jumla ya magoli 17 katika michuano hiyo msimu wa 2013/14.

Katika Tuzo hizo, Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew ameweza kuibuka na tuzo ya kocha bora wa mwaka, Mshambuliaji wa Colombia ‘James Rodriguez’ akitwaa Tuzo ya goli bora la mwaka, Mwanadada Nadine Kessler anayechezea timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa kike, Ralf Kellerman akinyakua tuzo ya kocha bora wa timu ya wanawake pamoja na  Hiroshi Kagawa akishinda tuzo ya urais bora wa mpira wa miguu.

Cristiano Ronaldo na Irina Shayk

Cristiano Ronaldo na mchumba wake Irina Shayk baada ya kuwasili katika sherehe za utoaji tuzo za Ballon D’or

Messi na kifaa chake Antonella

Messi na kifaa chake Antonella

James Rodriguez na kifaa chake

James Rodriguez na kifaa chake

Lionel Messi akiwasainia mashabiki wake

Lionel Messi akiwasainia mashabiki wake

Kipa wa Ujerumani na Bayern, Neuer akiwasaini mashabiki

Kipa wa Ujerumani na Bayern, Neuer akiwasaini mashabiki

Ronaldo na Marta wakipata uselfie

Ronaldo na Marta wakipata uselfie

Ronaldo akiwasainia mashabiki

Ronaldo akiwasainia mashabiki

Cristiano Ronaldo na Nadine Kessler wakipata ukodaki

Cristiano Ronaldo na Nadine Kessler wakipata ukodaki baada ya kukabidhiwa tuzo zao

Rais wa shirikisho la FIFA, Sepp Blater akimpingeza Ronaldo kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia

Rais wa shirikisho la FIFA, Sepp Blater akimpingeza Ronaldo kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia

Ronaldo akishangilia baada ya kutangazwa mshindi

Ronaldo akishangilia baada ya kutangazwa mshindi

Ronaldo akiwa amebeba Tuzo yake ya chezaji bora wa Dunia

Cristiano Ronaldo na kijana wake

Cristiano Ronaldo akimkabidhi kijana wake Ronaldo Jr tuzo yake ya mpira wa dhahabu

Joachim Low akisema machache baada y akukabidhiwa tuzo ya kocha bora wa mwaka

Joachim Low akisema machache baada ya kukabidhiwa tuzo ya kocha bora wa mwaka

Kikosi cha timu ya Dunia katika picha ya pamoja

Kikosi cha timu ya Dunia wakipata ukodaki

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s