POMBE YENYE SUMU YAUA WATU WAPATAO 60 MSIBANI NCHINI MSUMBIJI

Msumbiji

Picha hii haihusiana na habari

Watu wapatao 60 wamefariki Dunia katika jimbo la Tete nchini Msumbiji baada ya kunywa pombe ya asili inayosadikiwa ilikuwa na sumu.

Ofisa afya wa jimbo hilo, Alex Albertini amesema watu wengine 49 wamelazwa katika hospitali zilizoko katika wilaya za Chitima na Songo kaskazini mashariki mwa jimbo hilo.

Tukio hilo lilitokea msibani baada ya waombolezaji kunywa pombe hiyo iliyotengenezwa kwa mtama na maindi inayosadikiwa ilikuwa na sumu ya nyongo ya Mamba.

Nae Mkurugenzi wa afya wa jimbo la Tete, Kalimos amesema sampuli za damu zilizoathirika pamoja na pombe hiyo zimepelekwa katika hospitali moja mjini Maputo kwa uchunguzi zaidi.

Mwanamke aliyetengeneza pombe hiyo pamoja na ndugu zake ni miongoni mwa watu waliofariki Dunia.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s