KISANDUKU CHEUSI CHA NDEGE YA INDONESIA ‘AIR ASIA’ CHAPATIKA

Air Asia black boxWapiga mbizi nchini Indonesia wamekipata kisanduku cheusi kinachorekodi mwenendo wa ndege cha ndege ya shirika la Air Asia iliyoanguka kwenye bahari ya Java nchini humo.

Maafisa nchini Indonesia pia wanaamini kwamba wameweza kutambua kinasa sauti cha rubani ambacho ni sehemu ya pili ya kisanduku cheusi ingawa wapiga mbizi hawajaweza kukifikia.

Ndege ya shirika la Air Asia nambari QZ8501 ilipotea Desemba 28 mwaka jana kutokana na hali mbaya ya hewa ikiwa imebeba watu 162 wakati ikisafiri kutoka Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore inadhaniwa iko chini ya bahari ya Java.

Miili kadhaa ya watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo imekwishapatikana lakini miili mingi zaidi bado iko kwenye mabaki ya ndege hiyo ambayo bado haijapatikana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s