WATANO WAJERUHIWA KWA RISASI KATIKA SHOO YA CHRIS BROWN HUKO MAREKANI

 Chris Brown

Watu watano wameripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa mapema asubuhi ya leo(Jan.11) katika klabu ya usiku ya Fiesta iliyopo   San Jose, California nchini Marekani.

Tukio hilo lilitokea wakati mwanamuziki Chris Brown aki-perform jukwaani kibao chake cha Loyal katika party  iliyopewa jina la Capricorn Bash  ambayo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuwapongeza watu waliozaliwa kati ya mwezi Dec.22 na Jan.19 ambapo staa huyo alikuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo.

Mtandao wa San Jose Mercury umeripoti kwamba tukio hilo lilitokea majira ya 1:20 usiku kwenye barabara ya Monterey Kabla ya polisi wa doria kufika eneo la tukio na kukuta watu 4 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, wakati wengine watano wakikimbizwa hospitali jirani.

 Chris Brown amewajulisha mashabiki wake kuwa yupo salama salimini baada ya kuandika ujumbe mfupi kwenye ukurasa wake wa Twitter leo.  ”I’m”, aliandika Brown.

Polisi wamewaweka kizuizini watu kadhaa waliohusika kwenye shambulio hilo huku hali za majeruhi zikitajwa kuendelea vizuri.  Tazama tukio lilivyotokea hapo chini

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s