KIUNGO WA WOLFSBERG ‘JUNIOR MALANDA’ AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

Junior Malanda WolfsbergKiungo chipukizi wa timu ya Wolfsberg ya Ujerumani, Junior Malanda mwenye miaka 20 amefariki Dunia kwa ajali ya gari iliyogonga mti huko mjini phalian

Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Klaus Allofss amesema katika waraka wake kuwa watu wote wameguswa na kifo hicho na mshtuko mkubwa na hawaamini kama hawatakuwa nae chipukizi huyo waliyempenda kuwa nae lakini Mungu amempenda zaidi. na kuwataka familia  yake kuwa na subira katika kipindi kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.

Allofss ameongeza kuwa Malanda alikuwa mmoja wa wachezaji nyota na tegemeo kubwa kwa timu hiyo kutokana na kuwa na kipaji cha hali ya juu na mechi yake ya mwisho aliyocheza ilikuwa Desemba 20 mwaka jana, Wolfsberg iliposhinda mabao mawili kwa moja dhidi ya Coron.

Taarifa za polisi kutoka Wolfsberg zimesema kuwa Malanga alikuwa ni mmoja wa abiria katika gari lililopata ajali ya kugonga mti huko Belfed Jumamosi(Jan.10) na kufariki wakati akiwa katika msafara wa kwenda kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kusafiri kwenda nchini Afrika Kusini kuweka kambi.

Tayari wachezaji wenzake wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne, Thibaut Courtois na Eden Hazard wameandika katika mitandao yao ya Twitter walivyoguswa baada ya kumpoteza mchezaji mwenzao.

Junior Malanda aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Ubelgiji chini ya miaka 21 ameichezea Wolfsberg mechi 15 za Bundersliga msimu huu ikiwemo moja ya ligi ya Europa ya Everton ya England.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s