MTOTO WA JACKIE CHAN AFUNGWA JELA MIEZI SITA HUKO CHINA

Mtoto wa mwigizaji maarufu nchini China, Jackie Chan, Jaycee Chan amekutwa na hatia na kufungwa miezi sita gerezani kwa kosa la kutoa hifadhi na kuwaficha watuhumiwa wa dawa za kulevya nchini humo.

Jackie Chan Jayceen Chan

Jackie Chan(Kulia) na kijana wake wa kiume Jaycee(Kushoto)

Hukumu hiyo iliyotolewa katika mahakama ya jijini Beijing kufuatia sheria kali juu ya matumizi yasiyo halali ya madawa ya kulevya.

Jaycee mwenye miaka 32 aliwekwa kizuizini mwezi Agosti mwaka jana baada ya polisi nchini humo kugundua kiasi cha zaidi ya gramu 100 za bangi zikiwa nyumbani kwake.

Jaycee alikiri kosa na kusema ukweli kwa polisi mara tuu walipofika nyumbani kwake kwa sababu hakujua jinsi ya kukabiliana na masuala ya bangi na madawa ya kulevya.

Kukiri makosa kwa mtoto huyo wa muigizaji maarufu Dunia, inatoa ujumbe muhimu kwa serikali ya China kuwa hakuna mtu yeyote mwenye kinga juu ya sheria kali dhidi ya madawa ya kulevya nchini humo iliyoanza kutumika rasmi Juni mwaka 2014.

Mbali na kifungo hicho cha miezi sita, Jaycee pia atatozwa faini ya kiasi cha dola za kimarekani 322 kwa kosa hilo.

Baba yake ambaye aliyeuliwa na polisi wa China kuwa balozi wa kudhibiti mihadarati mwaka 2009, amesema kuwa kijana wake huyo amempa aibu na kumuhuzunisha kwa tukio hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s