YAYA TOURE ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA

Yaya Toure

Kiungo wa Kimataifa, Yaya Toure akizungumza mbele ya mashabiki lukuki baada ya kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure ameshinda Tuzo ya mwanasoka bora wa afrika kwa mara ya nne katika hafla ya utoaji tuzo kwa wachezaji bora zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria.

Toure mwenye umri wa miaka 31 aliteuliwa baada ya kucheza kwa kujitoa, akileta ushindi katika ligi kuu pia na kujitoa kuisaidia timu yake ya Taifa ya Ivory coast kuingia katika kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika baadae mwaka huu.

Toure amempiku mchezaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na Golikipa Vicent Enyama wa Nigeria.

Kiungo huyo wa Manchester City alipata jumla ya kura 175, Emerick kura 120 na Enyama alishika nafasi tatu kwa kupata kura 105.

Kwa ushindi huo unamfanya Toure afikie rekodi ya mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o ambapo kwa mara ya kwanza alishinda tuzo hizo mwaka 2011.

Utoaji wa tuzo hizo unafuatia kura zilizopigwa na makocha na wakurugenzi kutoka nchi wanachama wa shirikisho la soka barani Afrika ‘CAF’.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Toure amewashukuru wale wote walioshiriki katika upigaji kura.

Tuzo hizo ziliambatana na  burudani ya aina yake toka kwa wasanii nyota mbalimbali barani Afrika akiwemo msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye aliangusha shoo ya aina yake.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s