MAMA MTOTO WA LUDACRIS ATEMA CHECHE

LudaMama mtoto wa Ludacris amedai kitendo cha rapa huyo kufunga ndoa na mpenzi wake ni njama za kutaka kumchukua jumla mtoto aliyezaa nae ili aepuke kulipa gharama za dola 7000 kila mwezi.

Mtandao wa TMZ umesema kuwa mzazi mwenzie Luda, Tamika Fuller anadhani rapa huyo anataka kumhakikishia hakimu katika kuwania kwao haki na wajibu wa kufanya maamuzi kuhusu malezi ya mtoto kwa kuwa sasa yupo imara, ana nyumba yenye upendo …inayovutia kwa malezi bora ya mtoto tofauti na kulelewa na mzazi mmoja.

Tameka anasema anahofia huenda jaji akaona hoja rapa huyo kuwa na mashiko zaidi.

Mr & Mrs Bridges katika pozi siku ya ndoa yao

Mr & Mrs Bridges katika pozi siku ya ndoa yao

Luda alimchumbia mpenzi wake wa muda mrefu Eudoxie wakati wa mapumziko ya sikukuu za Christmas mwaka jana na kumuoa Christmas ya pili licha ya Tameka kudhani hizo zote ni njama tu.

Luda anatafuta kupewa kibali na mahakama ili aweze kuishi na mtoto wake wa kike aitwaye Cai mwenye umri wa mwaka mmoja.  Anadai yeye ni mzazi bora na anataka kumpatia maisha bora.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s