YANGA YAVUNJA MKATABA NA KASEJA

Juma KasejaUongozi wa klabu ya soka ya Yanga yenye maskani yake Jangwani,  umetangaza rasmi kuvunja mkataba na mlinda mlango wake nyota Juma kaseja.

Uamuzi wa kuvunja mkataba na Juma Kaseja umetangazwa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar.

Kaseja alisajiliwa na Yanga kwa kitita cha shilingi milioni 40 mnamo mwezi Novemba mwaka 2013 akitokea klabu ya Simba ya Dar es salaam.

Kabla ya kuchukua uamuzi huo, Kaseja anadaiwa kuwasilisha barua kwa viongozi wa Yanga akiomba mkataba wake uvunjwe kutokana na uongozi wa timu iyo kukiuka baadhi ya masharti waliyokubaliana awali.

Yanga imeamua kuachana na Kaseja wakati ikikabiliana na michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar usiku huu ikiwa Dimbani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s