WATU WENYE SILAHA ZA MOTO WASHAMBULIA OFISI ZA JARIDA LA VIKARAGOSI JIJINI PARIS NCHINI UFARANSA

Watu wanaodhaniwa kuwa ni maigaidi wamevamia ofisi za jarida moja la vibonzo na kufanikiwa kuuwa watu wapatao kumi na mbili Jumatano asubuhi(Jan.07) jijini Paris nchini Ufaransa.

20140108-PARIS2-slide-32SW-jumbo

Washambuliaji wakimweka chini ya ulinzi mmoja wa watu nje ya ofisi za jarida la Cherlie Hebdo

Miongoni mwa waliouwawa ni pamoja na mhariri wa jarida hilo la Cherlie Hebdo, wachora vibonzo watatu na maafisa wawili wa polisi.

Kanda moja ya video imeonyesha shambulio hilo ambapo wanaume wawili wakiwa na bunduki waliingia kwenye chumba cha habari na kuanza kuwafyatulia risasi waandishi wa habari hao wakati wakiwa kwenye mkutano.

Polisi wanasema washambuliaji hao kisha wakaanza kushangilia kwamba wamelipiza kisasi kwa niaba ya mtume kabla ya kutoroka kwa gari.

Gari hilo baadae limepatikana viungani mwa mji wa Paris na msako mkubwa wa polisi umeanza kuwatafuta wahusika huku mji mkuu wa Paris ukiwa umewekwa kwenye tahadhari sambamba na kuimarisha ulinzi katika maeneo ya ibada, mashirika ya habari pamoja na uchukuzi wa umma.

Cherlie Hebdo

Polisi akiangalia usalama nje ya ofisi za Cherlie Hebdo baada ya kutokea shambulio

Cherlie Hebdo

Kikosi cha waokoaji wakimpandisha majeruhi wa tukio hilo kwenye gari maalum la kubebea wagonjwa

France Newspaper Attack

Majeruhi akikimbizwa kwenye gari la wagonjwa

Cherlie Hebdo

Mmoja wa wafuasi wa dini ya kiislamu akiwa amebeba bango lenye kibonzo kinachomdhihaki mtume wao katika maandamano kupinga kitendo hicho

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s