IKULU YA MAREKANI YAMSAKA ALIYEVUJISHA SELFIE YA MTOTO WA RAIS OBAMA MTANDAONI

Baada ya kuzagaa kwa habari juu ya kuvuja kwa picha aina ya selfie kwenye mtandao wa Twitter kupitia akaunti ya Masked Gorilla ambayo alipiga mtoto wa Rais wa Marekani, Barack Obama, Malia Obama ikimuonyesha akiwa amevaa Tshirt ya Pro Era ambayo ni brand ya rapa maarufu wa Brooklyn, Joey Bada$$ imepelekea ikulu ya Marekani kuanzisha uchunguzi ili kuweza kubaini mtu aliyevujisha picha hiyo.

Malia Obama

Malia Obama akiwa ametupia kitu cha Pro Era

Kwa mujibu wa Fox News imeripoti kwamba ikulu ya Marekani inaangalia ni jinsi gani selfie hiyo ilivujishwa kwenye mtandao kwa mara ya kwanza huku  watu wakiwa hawana uhakika wa asilimia 100 kama picha hiyo ni ya kweli.

Michelle Obama ameweka sheria kali kwa binti zake kujihusisha na mitandao ya kijamii na huenda akawa hajapendezwa kabisa na kitendo cha picha iyo ya binti yake kutumika kwenye blogu za Rap na kupigia debe brand hiyo.

”Mimi bado  si muhumini mkubwa wa Facebook kwa matumizi ya vijana wadogo”, alisema Michelle wakati akihojiwa na mtangazaji Barbara Walters akielezea jinsi alivyowadhibiti mabinti zake, Malia na Sasha kujihusisha na mitandao ya kijamii.

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s