RICK ROSS AONYESHA MAPENZI KWA MIAMI HEAT BAADA YA KUCHORA TATTOO HII

Rapa na C.E.O wa lebo ya Maybach Music Group, Rick Ross ameonyesha mapenzi ya hali ya juu kwa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat inayoshirki ligi kuu ya NBA baada ya kuchora tattoo mpya ya moja kwa moja usoni kwake yenye logo ya timu hiyo.

Rick Ross

Rick Ross akionyesha Tattoo mbili mpya ambazo amechora usoni ikiwemo logo ya Miami Heat na brand ya Meek Milll  ‘DC’.

Rick Ross alikuwa ameongozana na lebo mate wake Meek Mill ambaye pia alichora nembo ya MMG kwenye kiganja cha mkono wake zoezi lililofanywa na duka la Unroyal Ink ambao ni wataalam wa uchoraji Tattoo.

Mapema katika msimu mpya wa ligi ya NBA, Ross alifanya uwekezaji mwingine mkubwa katika timu ya Miami baada ya kuiwekea dola 100,000 za kimarekani kama sehemu ya kuitabiria kumaliza msimu na rekodi nzuri kuliko Cleveland Cavaliers, kufuatia Lebron James kuhamia kwenye timu iyo akitokea kwao.

RR

Rick Ross akichorwa tattoo huku mkononi akiwa ameshika sigara kubwa

Rick Rozzay

Rozzay akionyesha Tattoo nyingine alizochora hapo awali

Meek Mill Tat

Meek Mill akionyesha Tattoo ya MMG ambayo amechora kwenye kiganja cha mkono wake

Meek Mill DC

Meek Mill na Rick Rozzay wakiwa wameunganisha mikono yao ikiwa ni ishara ya kusapotiana kwa kuchora Tattoo zenye logo zao – MMG na DC

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s